27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Geita washindwa kumaliza tatizo uhaba wa madawati

upungufu-wa-madawatiNA CHRISTINA GALUHANGA-DAR ES SALAAM

MKOA wa Geita unaogoza miongoni mwa mikoa saba kwa kuwa na upungufu mkubwa wa madawati.

Jambo hilo limetajwa kuirudisha nyuma juhudi za serikali katika   kuboresha elimu nchini.

Mbali na Geita, mikoa mingine ambayo haijakamilisha madawati ni Mwanza, Mara, Kigoma, Rukwa, Simiyu na Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa mikoa hiyo kuondoa kero hiyo vinginevyo wajitumbue wenyewe kwa kushindwa kuendana na kasi ya Rais  Dk.John Magufuli.

Simbachawene aliyasema hayo   Dar es Salaam jana wakati akipokea msaada wa madawati 3,500 yaliyotolewa na Benki ya NMB.

Alisema ni jambo la kusikitisha mikoa hiyo kushika nafasi za mwisho katika suala la kupatikana kwa madawati.

“Wapo wadau wengi ambao wameona umuhimu wa kuchangia elimu nchini lakini kwa mikoa hii inaonyesha jinsi ilivyofanya vibaya, nawaagiza hadi Januari wawe wamekamilisha upungufu huo vinginevyo viongozi wake wajing’oe wenyewe kwa sababu watakuwa hawawezi kuendana na kasi ya uongozi wa sasa,”alisema Simbachawene.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, alisema hadi sasa benki hiyo imekabidhi kwa serikali madawati 10,000   ambayo yamesambazwa katika shule 71 nchini za sekondari na msingi.

“Mkakati wa NMB ni kuisaidia serikali kuondoa changamoto ya wanafunzi kukaa chini, hivyo tuna imani wanafunzi watapata elimu kwa kiwango kinachostahili,”alisema Ineke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles