31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kashfa ya UDA yaibuka tena bungeni

bunge

Na Bakari Kimwanga – DODOMA

MZIMU wa sakata la uuzwaji wa hisa za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), umeibuka upya bungeni jana, huku Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), akitangaza kuwasilisha hoja binafsi ya kuomba kuundwa Kamati Teule ya Bunge.

Akichangia bungeni mjini hapa jana, Mdee alisema taarifa za kamati za kudumu za Bunge – Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na yeye kama Mjumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam hataki kuamini namna suala la UDA lilivyoibuka, huku baadhi ya wabunge wa CCM wakitaka halmashauri hiyo ivunjwe.

Alisema hoja hiyo ni kashfa kuhusu kiwanda hewa cha nyama na uuzwaji wa UDA, na kwamba hayo ni moja ya mambo ambayo wanapambana nayo ili kuondokana na ubabashaji huo.

“Ninataka kumwambia mzungumzaji kuwa anasahau kashfa hii ilitokea wakati Jiji likiwa chini ya CCM, ndiyo maana Jiji chini ya Ukawa tunataka tulisafishe ili halmashauri zile tatu na sasa zimeongezeka kuwa tano ziwe sehemu ya kuboresha jiji hili.

“Hawa wezi wanaotajwa wa Kamati kuhusu kashfa ya kiwanda cha nyama na UDA ni makada wa CCM na wanawajua, hatujaona popote wakipelekwa mahakamani,” alisema.

Alisema pamoja na hali hiyo, hivi sasa kikao cha Baraza la Madiwani kinakwenda kubatilisha maamuzi yenye dhuluma yaliyotokana na umiliki wa UDA.

“Naliambia Bunge msije mkathubutu, maana nimesikia mara zile Sh bilioni 5 alizolipa Simon Group zipangiwe matumizi, naomba niwaambie sisi kama Jiji tunatambua mamlaka yetu, sasa kama hatujitambui na Serikali inataka kuingilia, hatuwezi kutumia hii shilingi bilioni 5 kuhalalisha haramu kuwa kitu kitakatifu,” alisema

Alisema kwa bahati mbaya, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuona azimio la Baraza la Madiwani kugoma kutumia fedha hizo waligeuka na kwenda kuchukua kodi kwenye fedha za kifisadi.

“Suala la UDA, shirika lilianzishwa mwaka 1974 na Serikali ilikuwa na hisa 100, mwaka 1985 Serikali iligawa hisa zake asilimia 51 Jiji na yenyewe ikabaki na 49, hisa jumla ilikuwa milioni 15 katika hizo milioni 15, hisa milioni 7.5 ndiyo zilikuwa zimelipiwa, hisa zingine milioni 7.8 zilikuwa hazijalipiwa, kwa hiyo Serikali ilivyogawa hisa, Jiji ilipata milioni 3.3 na Serikali ikabaki milioni 3.4.

“Figisu zilianza 2001, UDA ilikuwa kama mashirika mengine, ilikuwa chini ya PSRC, kwa mantiki hiyo kisingewezekana chochote kwa maneno maneno hadi kwa gazeti la Serikali. Miamala yote iliyofanyika na UDA ilikuwa ni batili na katika muktadha huo, Jiji baada ya kwenda kwa Ukawa na kwa sababu tunasoma na kujiongeza, tumesema hili zoezi ni batili.” alisema Mdee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles