24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge wamchambua Trump

Donald Trump
Donald Trump

NA GABRIEL MUSHI, DODOMA

WABUNGE  wameelezea hisia zao baada ya mgombea urais wa Marekani kupitia Chama cha Republican, Donald Trump kushinda.

Wamesema ushindi huo ni funzo kubwa kwa serikali za Afrika ambazo huwa na mambo mengi wakati wa uchaguzi.

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), alisema  ushindi  wa Trump umeonyesha namna gani watu duniani walivyochoka na mifumo iliyozoeleka madarakani.

“Tusitazame uchaguzi wa leo (jana), tuangalie uchaguzi wa 2008, Rais Barack Obama alipoingia madarakani na matokeo ya kura za wananchi wa Uingereza walivyopiga kura za hasira za kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya, tukitazama yote tunaweza kuona mwenendo wa dunia.

“Uchaguzi huu unaonyesha namna gani watu walivyochoka kuongozwa na wale waliokua kwenye mifumo, wanataka mawazo mapya na mambo mapya.

“Pili inaonyesha taswira halisi ya siasa za ndani. Uchaguzi huu umeonyesha namna mfumo mzuri wa upigaji kura na utangazaji matokeo ulivyoandaliwa katika majimbo, kwamba kila jimbo linatoa matokeo yake.

“Niseme tu kwamba wale wametuacha mbali sana katika demokrasia, zaidi ya miaka 200… hatuwezi kuuona hapa Tanzania,” alisema.

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), alisema ushindi wa Trump ni wa kushangaza katika mazingira ya kawaida kutokana na mwamko uliokuwapo kuwa kura nyingi zilitabiri mshindi ni Hillary.

“Trump alighubikwa na kashfa mbalimbali, lakini ukichambua kwa kina zaidi ni kwamba wamarekani wamekuwa na kawaida ya kubadili vyama, si mara zote chama kutawala mfululizo kila mara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles