27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Utapeli wa kutumia majina ya viongozi washamiri Dar

sirooNA HERIETH FAUSTINE,DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa tahadhari kwa wakazi  wa jiji na wageni kuchukua tahadhari dhidi ya wahalifu wanaotumia majina ya viongozi wa serikali kujipatia fedha kwa njia ya  utapeli.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda Maalum, Simon Sirro, alisema hivi karibuni amepokea malalamiko kutoka kwa raia wa kigeni kutapeliwa na mtu asiyefamika, ambaye alijitambulisha kwao kwamba ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.

Alisema Oktoba Mosi mwaka huu, mfanyakazi wa Kampuni ya Group Six International aitwaye Marco Li(24),mkazi wa Mikocheni B,alipigiwa simu na mtu asiyefahamika  kwa namba 0719340914 na kujitambulisha kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Alimtaka atoe Dola za Marekani 3,500 kwa ajili ya msaada wa kusomesha mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Manila, Ufilipino.

“Baada ya kupata taarifa hizo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Group Six International, Jensen Hung (39), alikubali ombi hilo la Mkuu wa Mkoa feki na kumtuma msaidizi wake ambaye ni Marco aende kwa mkuu huyo  kujiridhisha.

“Alipofika kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa hakuweza kuonana naye badala yake alipiga simu kwa mkuu wa mkoa feki ambaye alimweleza yuko bize na shughuli nyingi.

“Marco alituma kiasi cha fedha cha zaidi ya Sh milioni saba katika benki ya Commercial iliyoko Mikocheni,”alisema Sirro.

Baada ya kutuma hizo fedha, Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuomba kwa Mkuu wa Mkoa feki amsaidie kumwidhinisha kuongezewa  muda wa kuishi nchini.

Alisema tapeli huyo alimtaka atoe   Dola za Marekani 7,000,ndipo Jensen Huang alimtumia zaidi ya Sh milioni 15 kupitia benki ya ECO.

“Oktoba 25 mwaka huu, Jensen Huang alipigiwa simu na Mkuu wa Mkoa feki na kumweleza suala lake la uhamiaji limekamilika na kutakiwa kutoa dola nyingine Marekani 5,000.

“Hapo ndipo walipogundua kutapeliwa baada ya kupiga simu kituo cha polisi kuhakiki namba ya simu na kugundua kuwa siyo ya Mkuu wa Mkoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles