27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Je, unataka kuoga ndani ya bakuli la supu?

3
Watoto wakiwa ndani ya bakuli la supu

 

NA JOSEPH HIZA,

JE, unaweza kuoga au kuogelea katika mlo au kinywaji ukipendacho ndani ya bakuli kubwa?

Jibu lako liwe ndiyo au hapana, nchini Japan kuingia ndani ya bakuli la mboga, supu au kinywaji ili kuogelea au kuoga humo ni jambo la kawaida mno.

Taifa hilo tajiri la Asia ni miongoni mwa yale ambayo kuna tamaduni au vitu vya kushangaza na kustaajabisha, ambavyo ni nadra mno kuviona katika nchi nyingine.

Utamaduni huo wa watu kuvinjari, kuoga au kuogelea ndani ya katika vyakula na au vinywaji una malengo makuu mawili; kupata tiba ya kiafya, urembo na kwa ajili ya kujifurahisha.

Katika taifa hili kuna nyumba au maeneo maalumu ya kuogea, yakiwa na bwawa la staili mbalimbali ikiwamo mfano wa bakuli au chupa.

Katika bakuli au chupa hizo kubwa kuna aina moja au mchanganyiko iwe wa supu, mchuzi, chai, vinywaji kama mvinyo na kadhalika, ambamo kwamo watu huingia na kuoga, kujisugua kwa vyakula au vinjwaji hivyo ili kufurahia maisha au minajiri ya kupata tiba fulani hasa ya ngozi ama urembo.

Ni aina ya maeneo ya kuogea au kwa maneno mengine mabafu, yakijulikana kwa jina la Spa, ambazo pia ni chemchem za mvuke zenye maji yenye madini na protein zilizowekwa au zinazotokana na vyakula au vinywaji tajwa.

Wengi wapendao kwenda kwenye chemchem hizi hutegemea pia kupata huduma kama vile kuchua na kukanda mwili au tiba nyingine  kama vile kuzamisha mwili au tiba vitobo (acupuncture).

Hata hivyo, baadhi ya chemchem  hutoa aina fulani zaidi ya huduma kama vile kuoga mvinyo, tiba za miguu au kuchua kwa kutumia mchuzi au cactus yaani dungusi kakati,  ambayo ni jamii ya mimea kama mpungate.

Chemchem ya Yunnesan huko Hakone, kwa mfano hutoa kwa wageni fursa ya kuchangamkia bwawa la mvinyo, chai, sake, kahawa na hata supu ya tambi.

Kwa taarifa sake ni aina ya mvinyo wa Kijapan uliotengenezwa kutokana na mchele, ambao unaaminika kuwa mzuri katika kutibu ngozi.

Kwa upande wa chai ya majani kujichovya kwayo kunaweza kuimarisha mfumo wa kinga mwilini.

Supu ya tambi maarufu kama ramen noodle, hupendelewa zaidi pia kwa vile ni moja ya vyakula vikuu na vipendavyo nchini humo.

Katika Spa ya Yunessan hutoa huduma ya kuoga supu ya tambi— ambapo wateja hujichovya na kujisugua kwa sababu zile zile iwe za kujifurahisha au kupata tiba.

Sambamba na hayo wakati mwingine huonja au kula mlo kabla ya kuingia ndani ya mabakuli haya, na wanasema huimarisha collagen na kuongeza metabolism.

Kwa taarifa collagen ni aina ya protein muhimu katika mwili wa binadamu, ambayo hupatikana kwenye mishipa ,mifupa,na tishu nyingine mwilini.

Protein hii ina asili ya nyuzi nyuzi inayounganisha na kusaidia tishu nyingine za mwili kama vile ngozi, mifupa, kano, misuli na mifupa laini.

Manufaa ya kuoga supu husaidia kupata ngozi changa, nyororo, nzuri kwa kila mtu anayeitaka.

Na ni wazi hilo linafanya kazi kwa sababu wengi wa wanaume wanaonekana kana ni wana miaka sita.

Wateja hujichovya wqenyewe katika maji yenye mchanganyiko na kuzigusisha miili yao na tani kwa tani za collagen.

Aidha, mchanganyiko unaweza kuwa wa radha ya maji ya pilipili ya rangi angavu, kahawia maziwa kama supu ya tonkotsu yaani supu ya mifupa ya nguruwe.

Kuhusu kuoga wine au bia, inaelezwa kuwa huwa na virutubishi vinavyoboresha ngozi ambavyo inasemekana kuwa na kilogramu mbili za collagen kwa kila chupa.

Kwa ufupi, sababu za watu wengi nchini humo kupenda aina hii ya uogaji katika mfano wa mabakuli au chupa kubwa za mlo au vinjwaji, utamaduni ambao unasemekana kuanzia miaka ya 2000 ni hizi:

Akijisugua kwa Tambi
Akijisugua kwa Tambi

Kuchangamsha

Kama ilivyo kwa spa nyingi, watu hujitokeza kulipia na kufurahia sikum kimwili na kiakili. Kwa mtu mwenye shughuli nyingi kunamaanisha kuwa na muda mchache wa kujimwagia haraka, hilo linamaanisha hawana muda wa kukaa na kujifurahisha na maji. Kuoga supu ya tambi kunatatua suala hili.

Kukutana na watu wapya

Kwa kuingia katika bakuli kubwa la supu, hasa ukijumuika na kundi la watu usiowajua katika bwawa, kunakufanya kujaribu vitu vipya. Katika hilo unaondoka ukiwa umepata marafiki wapya.

Kuimarisha ngozi

Mabakuli haya yana mchanganyiko wenye collagen inayoaminika kuimarisha ngozi na kuizuia dhidi ya sumu. Huruhusu seli za ngozi kufufuka na kukaa na afya.

Metaboliki

Baada ya umri fulani sehemu ya kubwa ya metaboliki hutoweka na iwapo si mtu wa mazoezi na hivyo kuoga supu husaidia kuimarisha metaboliki mwilini.

Lakini metaboliki ni nini? Ni jumla ya mabadiliko ya kikemikali na kimaumbile katika mwili hai wa binadamu. Ni mchakato ambao unaunganisha virtubisho na oksjeni ili kutoa nishati katika miili yetu ili iweze kufanya kazi ipasavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles