23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wavuvi haramu wajisalimisha

picwavuviNa Ally  Badi Kilwa

MSAKO unaondelea Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi dhidi ya wavuvi haramu, umesabbaisha watu 36 kujisalimisha kwa Mkuu wa Wilaya hiyo,Christopher Ngubiagai.

Hayo yalielezwa juzi na Ngubiagai alipozungumza na waandishi wa habari ofisi wake,mjini Kilwa Masoko.

Akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo,alisema msako huo ambao aliuita vita dhidi ya watu wasio na uzalendo,umesababisha wavuvi haramu kujisalimisha kwake nakuhaidi hawatarudia kufanya uhalifu huo tena.

Alisema tangu kuanza msako huo,baadhi ya wavuvi haramu wamesalimisha kwa wasamaria wema zana walizokuwa wanatumia katika kufanikisha uhalifu huo.

“Wamekuja kwangu nakuhaidi hawatarejea kufanya uhalifu na watashirikiana na serikali,nawaombawengine wafanye hivyo kabla hayajawakuta makubwa,”alisema Ngubiagai.

Alisema msako huo,umefanikisha kukamatwa zana mbalimbali zinazotumika kwa uvuvi huo unaotishia kuangamiza viumbe vya baharini na makazi yao.

mmoja wa wawavuvi haramu waliojisalimisha kwa mkuu huyo wawilaya,Gerold Fabiani,aliyekiri kuwa alikuwa anafanya uhalifu huo kwa takribani mwaka mmoja,alisema aliamua kujisalimisha kwa kuwa jina lake lilikuwa kwenye orodha ya wavuvi haramu katika wilaya hiyo.

“Orodha ya majina aliyonayo mkuu wa wilaya  ni sahihi,hakuna aliyesingiziwa na mimi ni miongoni mwa wavuvi haramu nakubali,kuanzia sasa nitasaidiana na Serikali kuwafichua wavuvi haramu,” alisema Fabiani.

Alisema sababu ya kujiingiza kwenye uvuvi huo, ni kuona wenzake walikuwa hawakamatwi na walikuwa wanapata samaki wengi kuliko yeye aliyekuwa anavua kwa njia halali.

Naye mvuvi Abdallah Ahmad,licha ya kufurahia na kuunga mkono kamatakamata hiyo, alitoa wito kwa Serikali ya wilaya  kufanya  misako mara kwa mara  ya kushitukiza.

Alisema uvuvi haramu umesababisha wavuvi wadogo kama yeye kushindwa kupata samaki.Kwa madai kuwa hana chombo cha kusafiria na kumfikisha bahari kuu.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Halmashauri ya Mamlaka ya Mji mdogo Wilaya ya Kilwa,Juma Mkomi, alisema licha ya Serikali kufanya doria mara kwa mara, inapaswa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu madhara ya uvuvi haramu,kulasamaki waliouwawa kwa sumu na faida za kulinda bahari na viumbe vilivyomo baharini kwa masilahi mapana ya kizazi cha sasa nakijacho.

“Na sisi wananchi kwa upande wetu tunawajibu wa kushirikiana na serikali,tuwafichue wanaoendesha vitendo hivyo,tuunde vikundi vya ulinzi na tusaidie kutoa elimu.Maana serikali bila kusaidiwa na wananchi haiwezi kufanikiwa,”alisema Juma Mkomi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles