25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

UNFPA yataja hatari zinazowakabili wasichana

Dk. Babatunde Osotimehin
Dk. Babatunde Osotimehin

Na MWANDISHI WETU – ZANZIBAR

RIPOTI ya hali ya idadi ya watu duniani ya mwaka 2016, inaonyesha kati ya vijana milioni 125 wa umri wa miaka 10, kuna wasichana milioni 60 waliotengwa katika sura ya dunia.

Imesema wasichana hao wanapewa fursa ndogo ya kukamilisha masomo kuliko wavulana katika kiwango cha sekondari na chuo kikuu.

Pia wana hatari zaidi ya kuwa katika hali mbaya ya afya ya mwili na akili kuliko wavulana na watapata tabu kutafuta kazi ya mshahara.

Akizungumza mjini hapa jana wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa UNFPA, Dk. Babatunde Osotimehin, alisema: “Zaidi ya nusu ya  wasichana wapatao milioni 60 wa umri wa miaka 10 wanaishi katika nchi 48 zenye ukosefu mkubwa wa usawa wa jinsia. Wanapewa fursa ndogo ya kumaliza shule kuliko wavulana.

“Wasichana wengi wako katika hatari zaidi ya kukabiliwa na ndoa za utotoni, ajira za watoto, ukeketaji na matendo mengine ya udhalilishaji.”

Alisema vitendo hivyo vya udhalilishaji ndivyo vinavyodhoofisha haki na afya ya msichana na kutishia matumaini ya ajenda ya maendeleo ya dunia.

“Vitendo hivyo huwafanya wasichana chini ya miaka 10 washindwe kutimiza ndoto zao kama wanawake na kuwazuia kuchangia katika maendeleo ya uchumi na jamii,” alisema Dk. Babatunde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles