24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kutana na mzazi anayeshirikisha wanae mazoezi ya yoga

1

WAKATI sehemu kubwa za familia duniani zikipendelea kukaa sebuleni zikitazama televisheni hali ni tofauti kwa Summer Perez, mama wa watoto wawili.

Yeye wakati kama huo huutumia na wanae wawili kufanya mazoezi ya viungo na pumzi maarufu kwa jina la yoga.

Pamoja na wanae Jayden mwenye umri wa miaka mitano na Cataleya (3), hushiriki mazoezi hayo na kuishirikisha jamii ili ijifunze kitu kutoka kwao.

Kwa sababu hiyo, Perez mwenye umri wa miaka 31 hushea picha zake katika ukurasa wake wa Instagram ambako ana wafuasi karibu 80,000 wanaomfuatilia.

Lakini yoga ni zaidi ya hobby tu kwa mkazi huyo wa Las Vegas, ambaye husifia kitendo hicho kwa kumsaidia kukabiliana na nyakati ngumu.

Mwaka 2013, nilijikuta nikiwa katika hali mbaya kisaikolojia na nilikata tamaa ya maisha kutokana na usongo ulionikabili,  aliandika katika ukurasa wake wa Go Fund Me.

Anasema kupitia mazoezi ya yoga, nimeweza kuzipita changamoto hizo kwa asilimia nyingi zikihusisha suala la kisaikolojia ambayo yaliniweka katika wakati mgumu na ambayo yalihatarisha mwenendo wangu wa maisha.

“Iliniondoa kutoka katika msongo na kusaidia kuwa na nguvu na mwepesi wa kimwili na kiakili,” anasema.

Perez aliandika katika blogu yake kwamba kuna faida nyingi za kufanya mazoezi na watoto.

“Ninawahusisha wanangu katika mazoezi, tunapata muda wa kujiweka karibu zaidi, kucheka pamoja na kujifunza vitu vingi.

“Hujifunza namna ya kufanya mazoezi na kufahamu umuhimu wake na kwamba si kitu cha ajabu kukifanya.

“Watoto wameanza kuelewa miili yao na wanachohitaji kuishi kwa amani na afya,” anaandika.

Perez hivi karibuni alianzisha ukurasa wake wa Go Fund Me kumsaidia kuchangisha fedha kukamilisha kozi yake ya mafunzo ya ualimu wa yoga.

Anaandika; “Kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, tumekuwa tukihaha kifedha, kitu ambacho kilisababisha mazingira mabaya.

“Ningependa kushea zawadi ya mazoezi ya yoga pamoja na manufaa yake na wengine waliowahi kuwa katika hali kama yangu ya mfadhaiko,” anasema.

Ana matumaini ya kusaidia wengine kwa masuala ya afya ya akili pamoja na wafungwa na watumiaji sugu wa mihadarati.

Pia anadai kusaidia wazazi kusaka njia nyingi zaidi za kuwekana karibu na watoto.

Yoga inakotoka na umuhimu wake kwa ufupi

Inasemekana yoga ni kitendo ambacho kina historia katika imani za Mashariki hasa katika maandishi, tamaduni na elimu katika jamii ya kale ya Indus.

Takribani zaidi ya miaka 3300 Kabla ya Kristo, watu walikuwa wanajifunza meditation yaani kutafakari kwa lengo la kukuza ujuzi wa kiimani.

Katika maandishi ya kale ya Kihindi kuna Sutras, ambayo ni mikoa 195 ya yoga iliyokuwa ikitumika hapo kale.

Watu wengi wamekuwa wakiangalia nje yao kutafuta furaha, nguvu, raha, tamaa n.k lakini imekuwa ni vigumu mtu kijiangalia ndani na kutafuta ukweli ndani yake.

Pia katika saikolojia imekuwa shida mno kwa watu kujifunza kujiongoza, wengi wamekuwa wakijiongoza kwa kufuata hisia, mawazo, homoni ambazo zinawatawala.

Mfano mzuri ni jinsi ya kufanya uamuzi mgumu hasa pale inapotokana na mazoea uliyojiwekea.

Moja ya dhumuni kubwa la yoga ni kuweza kurudisha ufahamu wako ndani mwako na kuweza kuunganisha mwili na akili kwa pamoja.

Kwa maneno mengine katika yoga unatakiwa kuweka akili yote kwenye pumzi na nishati ya mwili.

Mwili na akili pale vinapoweza kukutana unaweza kuamua utakavyo na unakuwa kiongozi wa maamuzi yako na kiongozi wa mawazo yako.

Pia unajifunza kuwa na furaha ya ndani, furaha ambayo haitegemei maisha, mali, hali, watu, au vitu vya nje bali ni furaha ya ndani, furaha isiyoweza kuibiwa na furaha ambayo ni ya milele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles