24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RC amuweka rumande saa 24 mhandisi wa maji

Vector illustration of a man lock up in prison

Na Raphael Okello

MKUU wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili amewaweka rumande kwa saa 48, Mkurugenzi    wa Mamlaka  ya Majisafi na Majitaka   Bunda (BUWSA), Mansour Mandeba   na Mhandisi Msaidizi, Maisha  Marechela,  wakidaiwa  kushindwa kutoa  huduma bora za maji  kwa wakazi wa Bunda.

Hao ni maofisa wa kwanza    kuchukuliwa hatua  katika mamlaka hiyo baada ya wakazi  wa   Bunda  kuilalamikia mamlaka hiyo  tangu mradi   mkubwa wa maji kuanza mwaka 2006.

Mandeba  na Marechela   wamewekwa ndani  kwa kudaiwa  kushindwa kutekeleza agizo  la mkuu huyo  wa wilaya  tangu   Agosti mwaka huu.

Agizo hilo liliwataka   kutoa maelezo ya kina  sababu  zilizofanya  mradi  mkubwa wa maji  uliogharimu takriban Sh bilioni tisa   kushindwa kuwapatia maji safi  wakazi wa mji huo.

Kabla ya kuwaweka ndani  juzi   saa 7.00 mchana,   Bupilipili alidai  kuwa  watumishi hao  ni wahujumu uchumi  kwa kuwatoza  wateja  wa maji  tozo  zilizo chini ya  kiwango  kilichoelezwa katika  mwongozo wa serikali na
kusababisha  mamlaka hiyo kutojiendesha  inavyotakiwa.

Alisema suala  la kukatika maji kila mara kutokana na uharibifu wa miundombinu ni tatizo sugu  linalowatatiza  wananchi.

DC alisema  mamlaka hiyo ina watumishi  wengi  wasiokuwa na tija na akashauri wapunguzwe.

Sababu  nyingine  ni  kutoweka wazi  kiwango  cha adhabu kinachotakiwa kutolewa   na wanaohujumu au kuharibu miundombinu ya maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles