23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Dunia:Umasikini waendelea kupungua duniani

bankNA HARRIETH MANDARI-DAR ES SALAAM.

RIPOTI ya Benki ya dunia kuhusu hali ya umaskini duniani iliyotolewa wiki iliyopita imeonesha kuwa umasikini umeendela kupungua pamoja na  ukweli kuwa hali ya uchumi ni mbaya duniani kutokana na kuongezeka kwa pengo kubwa la kipato katika jamii.

Hata hivyo ripoti hiyo imeshauri kuwa ipo haja kuwepo na usawa katika jamii na kutiliwa mkazo ili umaskini uweze kuisha na hivyo kuwezesha dunia kufikia malengo yake ya milennia ya kuondoa umaskini ifikapo mwaka 2030.

Hayo yameelezwa kwenye ripoti hiyo ‘Umaskini na ushirikiano kwa nia ya kupata maisha bora,’  ambayo  hutoa takwimu za hali ya umaskini duniani kila mwaka inasema karibu watu milioni nane duniani wanaishi kwa kiwango cha Dola 1.90 kwa siku mwaka 2010 ambayo ni sawa na watu milioni 100 idadi ambayo ni ndogo ya kundi hilo ambalo huishi katika umaskini uliokithiri kuliko ilivyokuwa mwaka 2012.

Hali hiyo ya umaskini uliokithiri imeonekana zaidi katika nchi za mashariki mwa bara la Asia, na Pacific  hasa nchi za China,  Indonesia, na India, ambapo nusu ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri wapo Kusini mwa jangwa la Sahara wakati theluthi iliyobaki wanaishi Kusini mwa bara la Asia.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa kati ya nchi 83 duniani, nchi 60 ambazo utafiti huo umefanyika, wastani wa asilimia 40 yao ni  watu wenye  kipato cha kati   ya mwaka 2008 na 2013.

“Ni vema kuona kwamba nchi nyingi zimefanikiwa kupunguza umaskini na kuinua ustawi wa watu kwa wakakti mmoja   pamoja na hali ya sasa duniani ambapo uchumi umetikisika”alisema Raisi wa Benki ya dunia, Jim Kim.Akaongeza kuwa iwapo hakutakuwa na jitihada za kuhamamsisha usawa kama njia mojawapo ya kukuza uchumi itachukua muda kufikia malengo ya millennia ya kupunguza umaskini ifikapo 2030.

Ripoti hiyo imesisitiza kuwa kutokuwepo kwa usawa kati ya watu duniani kumepungua kwa kiasi kikubwa tangu mwaka 1990.Hata kwa upande wa nchi  mbali mbali hali ni mbaya tangu mwaka 2008.

“Kwa mujibu wa ripoti, kati ya nchi 83 duniani, 34 kati yake    viwango vya pengo la kipato limeongezeka kwa kiasi kikubwa kati ya walio na kipato kikubwa zaidi kuliko kwa asilimia 40 ambao wako katika kipato cha chini. Na kati ya nchi zenye kipato cha chini zipatazo 40, kati yake, 23 uchumi wake umeshuka katika miaka ya hivi karibuni.

Ripoti hiyo ikatolea mfano nchi kama Tanzania, Brazil, Cambodia,  Mali, Peru, ambazo zimefanikiwa suala la usawa katika miaka ya karibuni ambapo utafiti umeona usawa huo kupitia sera bora, ambapo zinampatia watu wote uwezo wa  kujipatia kipato, kuweza kupata mahitaji yote muhimu, na pia kuboresha mikakati ya maendeleo ya muda mrefu.

Vilevile zimeweza kuboresha mazingira bora ya ajira, na hivyo kutoa fursa mbali mbali za maendeleo kwa wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles