33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bei ya mafuta duniani yaanza kupanda

Waziri wa Mafuta wa Iran, Bijan Zanganeh
Waziri wa Mafuta wa Iran, Bijan Zanganeh

ALGIERS, ALGERIA

BEI ya mafuta duniani imeanza kupanda baada ya Jumuiya ya Nchi Wazalishaji wa Mafuta (Opec), kukubaliana kupunguza kiwango cha uzalishaji mafuta kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minane.

Habari za kufikiwa kwa makubaliano hayo zimesababisha kupanda kwa bei ya mafuta ghafi kwa karibu asilimia sita.

Wanachama wa Opec wamekuwa wakilaumiana kusababisha mdororo wa bei ya mafuta kutoka na kushindwa kuwa na msimamo mmoja wa kudhibiti bei.

“Opec imechukua uamuzi wa kipekee leo,” Waziri wa Mafuta wa Iran, Bijan Zanganeh alisema.

Mawaziri wa mafuta wa nchi wanachama wamesema maelezo ya kina kuhusu mwafaka wa sasa yatajadiliwa kwenye mkutano mwingine utakaofanyika Novemba mwaka huu.

Uzalishaji wa mafuta utapunguzwa hadi mapipa 700,000 kwa siku, ingawa upunguzaji wa uzalishaji hautakuwa sawa miongoni mwa wanachama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles