33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali ya Sudan yadaiwa kutumia silaha za kemikali Darfur

Tirana Hassan
Tirana Hassan

KHARTOUM, SUDAN

SHIRIKA la Amnesty International (AI) limedai Serikali ya Sudan imekuwa ikitumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake eneo la Darfur, na kwamba watoto 200 ni miongoni mwa waliofariki dunia.

Vifo hivyo vinadaiwa kutokea kuanzia Januari mwaka huu.

Wale wanaoathiriwa na ‘moshi wenye sumu’ kutoka kwa silaha hizo hutapika damu, kupata matatizo ya kupumua na ngozi zao huchubuka.

Serikali ya Sudan imekuwa ikikabiliana na waasi kwa miaka 13 katika Darfur.

Hata hivyo, madhila ya raia hayajakuwa yakiangaziwa vya kutosha tangu mwaka 2004, wakati wasiwasi wa kutokea kwa mauaji ya halaiki ulipoifanya jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua.

Sasa, ripoti mpya ya AI inasema mashambulizi yaliyokuwa yakitekelezwa na Serikali ya Sudan dhidi ya raia wake yanaonesha hakuna chochote kilichobadilika, kwa mujibu wa Tirana Hassan, Mkurugenzi wa utafiti wa Amnesty wa Maeneo ya Mizozo.

AI linasema uchunguzi wa miezi nane umefichua kwamba Serikali ilitumia mbinu za kuteketeza kila kitu, kubaka watu, kuua na kurusha mabomu eneo la Jebel Marra, Darfur.

Walionusurika waliambia AI kwamba moshi wenye harufu isiyo ya kawaida ulitanda angani baada ya mabomu kurushwa.

Amnesty wamesema wametuma nakala ya ripoti hiyo kwa Serikali ya Sudan, lakini bado hawajapokea jibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles