23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yasogeza mbele ufungaji mashine vituo vya mafuta

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo.

NA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesogeza mbele tarehe ya ufungaji wa mashine za kielektroniki (EFPP) ambazo ni maalumu kwa vituo vya mafuta.

Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini changamoto zilizojitokeza katika zoezi hilo ambalo ukomo wake ulikuwa ni leo.

Akizungumza na MTANZANIA, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema katika kikao kilichoikutanisha Wizara ya Fedha na Mipango, TRA pamoja na Chama cha wamiliki na Waendeshaji wa Vituo vya Kuuzia Mafuta Nchini (TPSOA), wakakubaliana kusogeza mbele zoezi hilo hadi itakapotangazwa tarehe ya ukomo wake.

Alisema hivi karibuni Serikali iliviagiza vituo vyote vya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kuwa vimefunga mashine hizo hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi huu ili kuhakikisha mapato yake yanakusanywa kikamilifu.

“Baada ya kukutana na kujadili changamoto zilizojitokeza katika zoezi hili la ufungaji wa mashine za kielektroniki maarufu kama Electronic Fuel Pump Printer (EFPP), tumeamua kusogeza mbele zoezi hili hadi hapo tutakapowatangazia tena kwamba mwisho utakuwa lini.

“Tumetoa uamuzi huu ili kutoa nafasi kwa TRA kushirikiana na TAPSOA kutatua changamoto zilizojitokeza, pia wamiliki wote ambao bado hawajafunga mashine hizo wanatakiwa kuendelea kutumia zile za mkono (ETR) hadi hapo watakapofunga zile za EFPP,” alisema Kayombo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles