27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kalengo Kamwendo: Rubani kijana Afrika

rubani-mdogo-afrikaNa Markus Mpangala

AKIWA na umri wa miaka 21, Kalenga Kamwendo anaonekana mchangamfu na mwenye haiba ya kusisimua. Amekuwa kijana mtulivu na makini kila hatua yake kazini.

Umakini wake umekuwa ukivutia watu mbalimbali kazini na maisha yake nje ya kazi. Anapendwa na watu wengi mno, kiasi kwamba amezidi kushangaza, ni kwa namna gani anavutia watu wote hao.

Lakini Kamwendo ni miongoni mwa marubani wa ndege wenye sifa kubwa mno duniani. Kalenga ni rubani katika Shirika la Ndege la Proflight la nchini Zambia.

Aliipata kazi hiyo kufuatia mkakati wa kuwapa nafasi vijana katika shughuli za maendeleo nchini humo. Aidha, inaelezwa uongozi wa Proflight umekuwa ukiendesha mikakati ya kuvumbua vipaji vipya kwa vijana kila mara.

Kamwendo aliajiriwa kuwa rubani wa ndege za Proflight Agosti mwaka jana wakati akitimiza miaka 20. Kwa sasa ni miongoni mwa marubani wengine 36 walioajiriwa na Proflight ambayo hufanya safari zake kati ya Zambia na Malawi.

Kalenga alizaliwa eneo la Copperbelt lilipo katika mji wa Kitwe. Kamwendo alianza kuonyesha mapenzi yake kwa kazi ya urubani tangu akiwa shuleni. Alikuwa mwanafunzi mahiri katika masomo ya Hisabati, Fizikia na Kiingereza. Mwaka 2011 baada ya kuhitimu masomo ya sekondari alichaguliwa kujiunga na Chuo cha Urubani cha Forty Three (Forty Three Air School) kilichopo mjini Eastern Cape, Afrika Kusini.

Mwaka mmoja na miezi mitatu baadaye alifanikiwa kupata leseni ya kurusha ndege, licha ya kuwa kijana zaidi kwa umri wake. Kamwendo amefanikiwa kuendesha ndege kwa zaidi ya saa 500 akiwa angani tangu alipojiunga na Shirika la Ndege la Proflight la Zambia.

Mara baada ya kurusha ndege ya kwanza akiwa rubani, Kamwendo alisema: “Nilisisimkwa mno, sikutegemea hata kama siku moja nitakuja kuvaa sare za marubani. Nilikuwa naendesha ndege hiyo kwenda Kasama na nilitakiwa kufika sa10 jioni. Kulikuwa na tani nyingi za hisia kutoka kwa abiria waliponiona kijana mdogo nawaendesha. Walifurahi kuona umakini wangu.

Inaelezwa kuwa awali kijana huyo alipanga kuwa Mhandisi kama baba yake, lakini alibadilisha  mawazo kutokana na kipaji alichokuwa nacho.

KUBADILI MSINGI WA ELIMU

Akizungumzia suala la Rubani huyo, Mkufunzi wa Chuo Cha Ualimu Marangu, Benjamin Mbezi wilayani Moshi, alisema; “Hayo ndiyo matokeo ya kuwa na mfumo mzuri wa elimu, ambao tumeupigia kelele muda mrefu. Kwa Tanzania itakuwa ndoto kupata pilot (rubani) kwa umri huo kwani hadi kufika Chuo cha Aviation (Chuo cha Ndege) na masharti yao kuwa uwe umemaliza kidato cha sita tayari mtoto wa Kitanzania ana miaka 25 au zaidi.”

Nini tafsiri ya simulizi za Kalenga Kamwendo na maoni ya Mkufunzi Benjamin Mbezi? Jawabu ni kwamba utaratibu wa kuwalazimisha wanafunzi wasome masomo yote (takribani 12) hauwezi kuwaletea manufaa kwenye mambo ya msingi ya maishani.

Naamini kuwa mwanafunzi anatakiwa kuandaliwa utaalamu wake angali sekondari si kuutafuta akiwa amehitimu kidato cha sita au vyuo vya kati, kisha akimaliza chuo kikuu ndiyo anaanza kuufanyia kazi, huku tukifahamu unahitajika uzeofu.

Wabobezi wa fani huandaliwa wangali wadogo, kadiri wanavyojikita kwenye fani husika ndivyo wanavyokuwa bora na kuweza kuwa wavumbuzi au wajuzi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles