30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘Mabilioni Nicol lazima yarudishwe’

felix-moshaNA WAANDISHI WETU

HUKU matayarisho ya mkutano wa dharura wa wanahisa wa Nicol yakiendelea, Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Felix Mosha, amesema Sh bilioni nane zilizochotwa kwenye akaunti ya Nicol lazima zirudishwe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mosha alisema ili kuhakikisha fedha hizo zinarudi, aliwataka wanahisa  wote wa Nicol kuhudhuria mkutano wa wanahisa utakaofanyika Oktoba 12, mwaka huu Dar es Salaam.

Fedha hizo zimechotwa na wanaojiita menejimenti ya sasa ya Nicol ambazo haijulikani zimetumikaje.

Alisema fedha hizo zilizotolewa kwa udanganyifu kutoka kwenye akaunti ya Nicol NMB, ni lazima zieleweke zimeenda wapi.

“Ieleweke kwamba si tu wanaojiita menejimenti ya muda Nicol hawakuwa na mamlaka ya kutoa fedha hizo benki, lakini pia hawakuwa wanaendesha kitengo chochote Nicol kilichohitaji gharama za kukiendesha. Kwa hiyo, wanahisa wa Nicol  kuambiwa wangojee mahesabu, haina mantiki,” alisema.

Mosha alisisitiza kuwa mkutano huo ni muhimu kwani wanahisa wana matatizo mengi yanayoendelea kuwakumba wakati fedha zao zinaliwa na wajanja.

Alisema baadhi ya wanahisa wa Nicol wamefariki dunia kabla ya kuonja matunda ya walichowekeza au kupata hata fedha zao kwa matibabu waliyoyahitaji.

Alisema wanahisa wameshindwa kufaidika na uwekezaji wao kutokana na vurugu zilizoanzishwa kwa makusudi na wanaojiita menejimenti ya muda.

“Sasa ni dhahiri kwamba vurugu zilikuwa zinalenga wachache kufaidika kwa udanganyifu na hili jasho la wanahisa masikini na wa kipato cha chini, zimefika mwisho.

“Halafu leo, wanaokazana kuiteka Nicol kwa kutumia oda ya Mahakama Kuu ambayo Jaji aliandika imeghushiwa, ndiyo wanakiri kusema mkutano wa wanahisa wa kuzungumzia hiki kiasi kikubwa hivyo cha fedha zao, usifanyike kwa kudai kwamba anayeutisha, hana mamlaka na eti wao wanaotumia oda iliyogushiwa ndiyo wenye mamlaka,” alisema Mosha.

Mwenyekiti huyo wa bodi ya Nicol alisema yeye na bodi yake wako kihalali kwani walirudishwa na mahakama na amri hiyo haijawahi kutenguliwa na mahakama yoyote ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles