24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Waliofuja fedha za vijana, wanawake kukiona

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

Na ELIYA MBONEA, ARUSHA

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametangaza msako mkali  ikiwamo kuwachukulia hatua za sheria watendaji waliofuja asilimia tano ya fedha zinazotengwa katika bajeti kusaidia vijana na wanawake katika halmashauri.

Akizungumza mjini hapa jana na vijana wajasiriamali na wasanii zaidi ya 200 wanaoendesha shughuli zao jijini hapa, alisema serikali haiko tayari kuona vijana waliopangiwa bajeti ya kusaidia kuendesha shughuli zao wakikwamisha na watu au kikundi cha watu wachache.

Alisema ni dhamira ya serikali kuona kila aina ya rasilimali inayopatikana nchini inawanufaisha wananchi na kuwaletea maendeleo hivyo hapatakiwi kuwapo na sababu yoyote ya kushindwa kufanya hivyo.

“Niwaagize Halmashauri ya Jiji la Arusha kuhakikisha asilimia kubwa ya fedha zinazopatikana zinakwenda kuwasaidia wananchi wa Arusha na si vinginevyo.

“Nitaandaa ratiba ya kutembelea kila kata za Jiji la Arusha   kukagua na kujionea hizi fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuwasaidia vijana na wanawake zimetumika inavyotakiwa,” alisema Gambo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles