23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mfahamu Shimon Perez, Rais wa zamani Israel aliyeiachia Dunia majonzi.

str1705interview_385040k

TEL AVIV, ISRAEL

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Israel aliyewahi kuhudumu pia kama Rais, Shimon Peres, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.

Aliugua kiharusi wiki mbili zilizopita na hali yake ikawa mbaya zaidi juzi Jumanne.

Peres, ambaye alikuwa mmoja wa viongozi waliobakia kutoka kwenye kizazi cha wanasiasa walioshiriki kuundwa kwa taifa la Israel mwaka 1948, alihudumu kama waziri mkuu wa nchi hiyo mara mbili na mara moja kama rais.

Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1994 kwa mchango wake katika mashauriano yaliyopelekea kutiwa saini kwa mkataba wa amani kati ya Israel na Palestina mwaka mmoja kabla.

Wakati fulani, aliwahi kusema kwamba Wapalestina ndio ‘majirani wa karibu zaidi’ wa Waisrael na wanaweza kuwa ‘marafiki wa karibu zaidi’.

Peres amefariki akitibiwa katika Hospitali ya Sheba karibu na mji wa Tel Aviv mapema jana, baada ya kulazwa akiwa mahututi alipopatwa na kiharusi Septemba 13 mwaka huu.

Rais wa Marekani, Barack Obama, amemwelezea Peres kama ‘rafiki wa karibu’ kwenye taarifa na akasema: “Aliongozwa na maono ya heshima na utu na alifahamu kwamba watu wenye nia njema wanaweza kustawi pamoja.”

Peres alikuwa waziri wa ulinzi wakati kikundi cha Wapalestina kilipoiteka ndege ya Israel na kuielekeza hadi Entebbe, Uganda mwaka 1976. Ndiye aliyeongoza juhudi za kuwaokoa zaidi ya mateka 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles