33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwigulu: Polisi wakamateni wanaowakejeli

mwigulu1Na RAMADHAN LIBENANGA, MOROGORO

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaokejeli vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Nchemba aliyasema hayo jana wakati akizungumza na askari polisi, askari magereza na askari wa idara ya uhamiaji mkoani hapa ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo.

“Watu wanaoongoza kwa uzalendo ni walioko katika vyombo vya usalama kwa sababu vinamlinda mtu aliyelala na mali zake.

“Lakini pia, ikitokea askari kavamiwa na majambazi kauawa au wameuawa, eti unakuta mtu anakejeli na kusema wangekufa ishirini ndio ingekuwa bomba.

“Kejeli kama hizo si za kuvumilika na mtu atakayefanya hivyo katika mitandao ya kijamii au mahali popote, anatakiwa kukamatwa na kuchukuliwa kama sehemu ya wahalifu wanaofanya makosa na si kwa mujibu wa sheria za mitandao.

“Anayeshangilia alichofanya adui na yeye ni sehemu ya adui, wakamatwe wafundishwe, lazima askari wapate heshima inayostahili,” alisema Nchemba.

Pamoja na hayo, waziri huyo alivitaka vyombo vya usalama vinapopambana na wahalifu, viwe vinatumia nguvu ili viweze kufanikiwa.

“Mnapopambana na wahalifu tumieni nguvu na nawaambia siungi mkono askari anayejihusisha na matukio ya uhalifu.

“Nawaomba pia mfanye kazi kwa kutenda haki ili wananchi wasiendelee kulalamikia vyombo vya dola kwamba vinaupendeleo na vinawaonea baadhi ya watu,” alionya.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Dk. Kato Rugainunura, alisema Gereza la Mahabusu Morogoro na magereza ya wilaya za Ulanga na Kilosa, yanakabiliwa na msongamano wa mahabusu.

Naye Ofisa wa Idara ya Uhamiaji, Mkoa wa Morogoro, Safina Muhindi, alisema idara hiyo inakabiliwa na tatizo la uwepo wa wafungwa wa nje ya nchi wanaomaliza muda wa vifungo vyao nchini kwa kuwa hawana bajeti ya kuwasafirisha kurudi kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles