30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Vituo vya polisi kujengwa kila kata Mbeya – RPC

rpc1

Na Pendo Fundisha, Mbeya

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, limewaagiza wakuu wa polisi wa wilaya kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi vya kata.

Agizo hilo lilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, wakati akijibu swali la MTANZANIA kuhusu mikakati ya jeshi hilo katika kupunguza au kutokomeza vitendo vya uhalifu kwenye maeneo ambayo bado huduma ya polisi haijafika.

Kamanda Kidavashari alisema Serikali imeweza kufikisha malengo yake ya huduma ya afya kwa Watanzania ili kuwapunguzia mzigo wa kutembea mwendo mrefu kupata huduma kwa kujenga vituo vya afya kwenye kila kata, hivyo ni vema pia huduma ya polisi ikaimarishwa kwa kujengewa vituo vya polisi kila kata.

Alisema tafiti zinaonyesha kuwa matukio ya uhalifu yanakuwa kwa kasi kubwa vijijini ambako miundombinu ya kipolisi bado haijafika, hivyo wameliona hilo na kulifanyia kazi kwa kuwafikishia huduma wananchi.

“Yapo maeneo ambayo tayari yametengwa kwa Mkoa wa Mbeya, mfano, Kata ya Igurusi, Ruwila, Mapogolo ambayo ukiangalia katika takwimu matukio ya uhalifu yapo juu na huduma za kipolisi zipo mbali, hivyo baada ya wananchi kupewa elimu wameonesha nia ya kujenga kituo cha polisi na tayari wametoa maeneo ya ardhi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles