23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

De Bruyne aumia, kuikosa Celtic

Kevin de Bruyne
Kevin de Bruyne

MANCHESTER, ENGLAND

KIUNGO  mshambuliaji wa timu ya Manchester  City,  Kevin de Bruyne, huenda akaukosa mchezo wa  Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Celtic,  baada ya kupata  jeraha katika  mchezo dhidi ya Swansea  ambapo timu yake  ilipata  ushindi wa mabao 3-1.

Mbelgiji  huyo mwenye thamani ya  pauni milioni  56, jana alitarajia  kufanyiwa uchunguzi wa jeraha lake baada ya kulalamika maumivu  makali  ya mguu katika mchezo huo.

Hata hivyo, kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola, hajawa na wasiwasi kumkosa nyota huyo wakati wakisafiri kuelekea  jijini Glasgow, Scotland.

Kocha huyo alisema kutokana na namna ambavyo nyota wake alivyokuwa akilalamika, inaonekana wazi alipata jeraha ya nyama za paja.

“Sijajua jeraha hilo litakuwa kubwa kwa kiasi gani kwa  kuwa mimi si daktari, tukifika Manchester atapatiwa uchunguzi ili kufahamu  kitu kinachomsumbua.

“Nasikitika sana kwani  Kevin ni mchezaji  muhimu katika timu yetu,  hiyo ndio sababu ya kuwa na kikosi kipana,” alisema Guardiola.

Manchester City iliwafunga  kwa mara ya pili ndani ya wiki moja timu ya Swansea baada ya kuwafunga  mara ya kwanza katika mchezo wa Kombe la  Ligi ya England (EFL).

Mshambuliaji wa timu hiyo, Sergio Aguero, alifunga mabao mawili katika mchezo huo wa EFL.

Aguero kwa sasa amefunga mabao 11 katika michezo sita msimu, huu hata hivyo  Guardiola anataka nyota huyo kujituma zaidi uwanjani.

Kocha huyo  alimpongeza  nyota huyo baada ya ushindi huo na kumweleza kuwa anaweza  kufanya vizuri zaidi ya ushindi wa mabao hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles