28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi: Tutawatia mbaroni walioua askari

SSSAsifiwe George na Juma Hezron (TSJ), Dar es Salaam,
JESHI la Polisi limesema linaendelea na msako mkali wa kuwabaini watu wanaodaiwa kuhusika na tukio la kuuawa kwa askari polisi wawili wilayani Rufiji.
Watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi, walivamia Kituo cha Polisi Ikwiriri ambapo waliua askari wawili na kuiba silaha.
Akizungumza na MTANZANIA, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja, alisema pamoja na kuendelea na kazi hiyo, lakini kwa sasa hawezi kuzungumza kwa undani tukio hilo kwani anaweza kuharibu mwenendo wa uchunguzi.
“Kwa kweli siwezi kusema lolote kuhusu operesheni hii kwa sababu tunaweza kuharibu upelelezi wetu, hivyo kuweni wavumilivu tutakapokamilisha tutatoa taarifa kwa vyombo vya habari ili wananchi watambue tulichokipata katika uchunguzi wetu,” alisema Chagonja.
Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ameahidi kutoa zawadi ya Sh milioni 20 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa na hatimaye kupatikana kwa silaha zilizoporwa na majambazi hao.
Tukio hilo lilitokea Januari 20 saa nane usiku katika Kituo cha Polisi Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani ambapo askari wawili; Koplo Edgar ambaye alikatwa mapanga na WP Judith aliyepigwa risasi katika ubavu wa kulia na kutokea upande wa kushoto wote walifariki dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles