24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali za mabasi zaua 254

pg-2

NA RAYMOND MINJA, NJOMBE

WIMBI  la ajali limezidi kumaliza maisha ya Watanzania, baada ya kutokea ajali 237 na kusababisha vifo vya watu 242 tangu Januari hadi Agosti, mwaka huu. MTANZANIA linaripoti

Habari za uhakika kutoka makao makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani, Dar es Salaam zinasema mbali ya vifo hivyo, ajali hizo pia zimesababisha majeruhi 885.

“Ukiangalia takwimu hizi, utaona watu wengi wanapoteza maisha kutokana na ajali hizi, lazima kila mmoja wetu azikemee.

“Fikiria hizi ni ajali za mabasi ya kwenda mikoani pekee…tunawaomba abiria wote wanaotumia mabasi haya kutoa taarifa kupitia namba za simu za kiganjani zilizobandikwa ndani ya mabasi,”alisema ofisa mmoja wa kikosi hicho ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Alisema ajali hizo, zimehusisha mabasi 267 ambayo kila siku yanasafirisha abiria kwenda mikoa mbalimbali.

NEW FORCE

Wakati huo huo, watu 12 wamefariki dunia na wengine 28 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya New Force walilokuwa wakisafiria kupata ajali.

Ajali hiyo ilitokea juzi ikihusisha basi lenye namba za usajili T 429 DEU lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda mjini Songea, mkoani Ruvuma.

Akizunguma na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Njombe Prudensiana Protasi, alisema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Charles Chilwa na kwamba ilitokea saa 1.30 usiku katika Kijiji cha Lilombwi, Kata ya Kifanya, barabara kuu ya Njombe- Songea.

Kwa mujibu wa Kamanda Protasi, miongoni mwa waliofariki dunia, wanane ni wanawake na wanne ni wanaume.

“Kwa hiyo, majeruhi 10 wamelazwa Hospitali ya Kibena na wengine wamepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.

“Majeruhi 16 walitibiwa Kibena na kuruhusiwa,wengine 12 wamelazwa hospitalini hapo wakiendelea na matibabu,” alisema Kamanda Protas.

“Hata hivyo, miili sita kati ya 12, tayari imetambuliwa na taratibu za kuchukuliwa na ndugu zao, zimeanza kufanyika na mingine sita bado haijatambuliwa.

“Hadi sasa tunaendelea kumsaka dereva wa basi hilo, kwani baada ya ajali hiyo alitoroka,” alisema.

Mmoja wa abiria waliokuwa kwenye basi hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendo kasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles