33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM Mkoa wa Arusha hali si shwari

Shaka Hamdu Shaka
Shaka Hamdu Shaka

Na ABRAHAM GWANDU, ARUSHA

HALI si shwari ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha, ambapo wanachama wa umoja huo wamelazimika kufunga ofisi za  kwa makufuli wakishinikiza aliyekuwa katibu wa umoja huo, Ezekiel Mollel, kukabidhi ofisi kwa katibu mpya .

Tukio la kufunga ofisi za umoja huo lilitokea jana ambapo chanzo chake baada ya kikao kufanyika juzi saa nne usiku, kutokana na Mollel kugoma kukabidhi ofisi kwa katibu mpya  Said Goha, ambaye amehamishiwa mkoani humo akitokea mkoani Lindi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika eneo la ofisi za jumuiya hiyo, baadhi ya wanachama wa UVCCM walisema kuwa kitendo cha Mollel ambaye alishapokea barua ya uhamisho kugoma kukabidhi ofisi ni utovu wa nidhamu.

“Tumeamua kufunga ofisi kwa sababu hatuwezi kukubali kitendo alichofanya Ezekiel, yeye amehamishwa kama hakubaliani na uhamisho zipo taratibu za kufuata au anaweza kuandika barua ya kuacha kazi si kung’ang’ania ofisi” alisema Ibrahim Ibrahim .

Pamoja na kulaani kitendo cha Mollel kukataa kutoka ofisini, Ibrahim alimshutumu Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa,  Lengai ole Sabaya kwa kumpotosha katibu huyo.

“Sabaya na Mollel wameifanya ofisi yetu (UVCCM) kama mali yao binafsi , wanaamua vile wanavyotaka bila kufuata utaratibu wa vikao , majadiliano kiasi cha jumuiya yetu kudharaulika machoni mwa jamii.

“Haiingi akilini kiongozi unapata uhamisho unagoma, wewe ni nani ndani ya UVCCM ? hii ni hatari sana CCM inapaswa kuliangalia hilo kwa jicho la kipekee bila kuonea mtu wala kupepesa macho’’ aliongeza .

Akizungumzia tuhuma hizo, Mollel alisema vijana waliojiita wanachama wa  UVCCM na kufunga ofisi za jumuiya hiyo mkoani Arusha ni wahuni na hawana madaraka wala wadhifa wowote ndani ya jumuiya hiyo.

“Najua hizi ni jitihada za kujaribu kuficha madudu yanayoendelea , nitawasilisha taarifa ya kamati ambayo mimi ni mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji ya mkoa na si kwa katibu mpya aliyekuja ili kulinda uoza unaofanyika,” alisema.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai ole Sabaya alifika jana mchana katika ofisi hizo na kuamuru minyororo na kufuli zilizowekwa kuvunjwa ili kuruhusu shughuli nyingine za jumuiya ziendelee.

Ilipofika mchana jumuiya hiyo ilitoa taarifa ya kumsimamisha kazi Mollel kwa kutotii agizo la makao makuu linalomtaka kuhama na kusibabisha mvutamo na malumbano yasiyo na tija kwa Chama Cha Mapinduzi  Mkoa wa Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema kuwa hatua hiyo inatokana na Mollel kukaidi agizo la kutakiwa kukabidhi ofisi kwa utaratibu lakini badala yake amegoma.

Alisema tangu Agosti 25, mwaka huu makao makuu ilimwandikia barua Mollel ya kumuhamishia  Makao Makuu  Dar  es Salam, lakini cha ajabu kwa muda wote amekuwa akikaidi kuhama kwa sababu zake binafsi.

Alisema kikao cha Sekreterieti ya Taifa kilichoketi Septemba 14, kimeamaua kumsimamisha kazi katibu huyo na kumtaka ampishe katibu mpya wa Mkoa, Said Goha aliyehamia Arusha akitokea Lindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles