30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Nissan yapanua soko magari mapya nchini Tanzania

7388

Na Joseph Lino,

Nissan Tanzania inasema soko la magari  mapya nchini  ni nzuri  ukilinganisha  na kushuka kwa biashara ya magari baadhi ya nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara.

Mkurugezi wa Nissana Tanzania,Christophe Henning aliongea na Mtanzania kuwa Tanzania kuna soko huru la magari inayosababisha changamoto nyingi katika uuzaji.

Kampuni hii inashikiria asilimia 12 au nafasi ya tatu katika soko la magari mapya nchini. Nissan imefungua showroom mpya ya magari jijini ikiwa kuongeza wigo katika biashara ya magari nchini.

Nissan huuza magari mpya kati ya 3,000 hadi 4,000 kwa mwaka ambapo magari mengi inayouza kuwa ni modeli ya  VX na pickup ya tani moja.

Katika soko la magari ya abiria, Tanzania soko linashikiriwa na magari yaliyotumika hasa kutoka Japan.

Magari ya Nissan hapa huwa yanasambazwa na  Associated Motor Holdings (AMH) ambayo inashikiriana na kampuni ya Imperial ya nchini Afrika Kusini ambao pia ni wauzaji wa magari nchi za  Kenya, Zambia na Malawi.

Imperial ni kampuni ya magari inawakala 250 katika nchi 40 za bara la Afrika na kuuza magari zaidi ya 200,000 kila mwaka.

Mkurugezi wa AMH Africa, Tim Jaques anasema  “NISSAN ni bidhaa  inayojulikana dunia nzima ambayo imewawezesha kwenda Afrika Mashariki na ili kuendana na hili tumewekeza vizuri kanda hii na kutakuwa uwekezaji zaidi kwa baadae kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa katika soko la Tanzania,’’

“Hii sio katika miundombinu yake  lakini pia katika ajira, mafunzo na maendeleo ya kijamii, kushirikiana na Nissan tunategemea kutumia uwezo wetu kwa kuwapa wateja huduma bora,”

Mkurugezi wa mauzo wa Nissan South Africa, Jim Dando anasema kampuni yake italeta wataalamu wa usafirishaji pamoja na magari mpya na vifaa vyake ili kuimarisha soko lake nchini.

Kampuni ya Nissan inashika nafasi ya sita duniani katika utengenezaji wa magari, na imekuwepo hapa Tanzania kwa miaka mingi kupitia wakala wake DT Dobie na CFAO Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles