25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Enrique ajibebesha zigo la lawama, Barcelona

Luis Enrique
Luis Enrique

BARCELONA, HISPANIA

KOCHA wa timu ya Barcelona, Luis Enrique, amesema hatolaumu  kiwango cha  wachezaji wake baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu   iliyopanda daraja msimu  huu,  Deportivo Alaves katika Uwanja  wa  Nou Camp, Barcelona.

Enrique alibainisha kuwa uwezo wa wapinzani wao ulikuwa wa hali ya juu  kutokana na kutumia mbinu iliyowabana na kushindwa kupata bao.

Hata hivyo,  Enrique   alisema  alipata  mshtuko  baada ya  timu hiyo iliyopanda daraja  kuwafunga mabao  hayo wakiwa  uwanjani humo.

Katika mchezo huo,  kocha huyo  aliwaweka benchi  wachezaji wake mahiri, Lionel Messi  na   Luis Suarez  wakisubiri mchezo wa  Ligi ya Mabingwa  Ulaya dhidi ya  timu ya  Celtic utakaochezwa wiki ijayo.

Kocha huyo alimwanzisha Neymar Jr ambaye  alirejea katika michuano ya Olimpiki yaliofanyika jijini Rio de Jeneiro, Brazil.

Mbali na Mbrazili huyo, Enrique  alikuwa akitambulisha wachezaji wapya  akiwamo Ibai Gomez  ambaye  hakuwa na mafanikio mazuri  katika mchezo huo.

Enrique alithibitisha kwamba kocha wa timu ya Deportivo Alaves, Mauricio Pellegrino, alifanikiwa kimbinu.

“ Tunastahili lawama  lakini kwa upande wetu tulikuwa hatuna namna ya kupata ushindi  kutokana na  ubora wa wapinzani wetu.

“Katika suala zima la ushindi  inategemea na  kiwango cha wachezaji tegemezi , lakini baada ya kufungwa  anayelaumiwa ni kocha,” alisema.

Kocha huyo alidai kwamba anastahili lawama zote na kuahidi kurekebisha makosa yaliyojitokeza baada ya kushuhudia timu yake ikipata kipigo hicho.

“Mimi ni kiongozi wa kilichotokea, mabadiliko yaliyofanyika ndio chanzo cha  kupata matokeo mabovu,  hata hivyo  nitajitahidi kukiboresha kikosi changu,” alisema Enrique.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles