30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kujenga nyumba nje ya nchi

NA ESTHER MBUSSI, DODOMA

SERIKALI inakusudia kujenga nyumba katika balozi zake nje ya nchi ili kupunguza gharama ya pango katika nchi wanazowakilisha.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima.

Adam Malima
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima

.

Alisema Serikali imefanya uamuzi wa makusudi kujenga nyumba hizo kutokana na kuwapo kwa viwanja vingi katika nchi hizo.

Alisema viwanja hivyo vilivyopo katika nchi za India, Ethiopia, Misri na kwingine vitasaidia kupunguza matumizi  katika majengo ya ubalozi nje ya nchi kwa kuwa ina viwanja sehemu nyingi badala ya kila mwaka kukodisha.

“Tuna viwanja nchi nyingi badala ya kila mwaka kutumia shilingi milioni 14 hadi 15 katika pango ni afadhali tuanze kujenga huko, balozi anapopanga nje huwezi kuacha kumtumia fedha,” alisema Malima.

Alisema Serikali itatengeneza mfumo kudhibiti nidhamu katika matumizi ya fedha za umma.

Alisema vitu kama mbegu na mbolea katika sekta ya kilimo ni muhimu kwa sababu asilimia 70 ya Watanzania uhai wao unatokana na kilimo, hivyo Serikali imedhamiria kufanya mabadiliko katika sekta hiyo.

“Tuna taasisi tatu za udhibiti wa mbolea, udhibiti wa dawa lazima tuhakikishe taasisi hizo zinapewa fedha za kutosha ili watu wasijitengenezee utajiri.

“Kuhusu uwekezaji wa miradi mikubwa, tumezungumzia miundombinu, reli, barabara na mawasiliano lakini kubwa zaidi ni kuhusu sekta ya umeme.

“Kwamba kwa mwaka huu, Serikali ipunguze matumizi yake katika nishati ya umeme na tuweze kuangalia utaratibu wa kukaribisha sekta binafsi kwa sababu tunatumia mabilioni ya fedha katika umeme sasa pale sekta binafsi itakapoingia ndiyo utaratibu wa nchi nyingine,” alisema Malima.

Kuhusu nafasi ya taasisi za fedha katika maendeleo ya nchi, alisema Serikali imekubaliana kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kufanya tathimini ya kiasi gani taasisi za fedha zinaweza kuchangia fedha nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles