23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tabora: Wanafunzi 170 wasoma darasa moja

wanafunzi

Wanafunzi 172 wa Shule ya Msingi Mwinyi katika Manispaa ya Tabora  hulazimika kutumia chumba kimoja cha darasa kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa shule hiyo, Simon Toyi, shule ina  wanafunzi 1721 huku vikiwapo vyumba vya madarasa 10.

Toyi alisema shule ina upungufu wa   vyumba 20 vya madarasa  kuweza kutosheleza wanafunzi wote   ikiwa ni   wastani wa kila darasa kuwa na wanafunzi 45.

Alisema shule pia inakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo 37 ambako kwa sasa kuna matundu 10  na mahitaji yakiwa 47.

Toyi aliongeza kuwa hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha maendeleo ya elimu shuleni hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles