27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Walikuwa na mchango mkubwa Man City, sasa thamani yao imeshuka

yaya na hart

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO,

KATIKA mafanikio makubwa ya klabu ya Manchester City ya hivi karibuni, kuna baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa na mchango mkubwa na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo kuweza kutembea kifua mbele kwa watani wao na wapinzani Manchester United katika jiji la Manchester.

Manchester United kwa mara ya mwisho kutwaa taji la Ligi Kuu nchini England ilikuwa msimu wa mwaka 2012-2013, huku timu hiyo ikiwa chini ya kocha Aleix Ferguson, lakini msimu uliofuata wapinzani wao walifanikiwa kuchukua taji hilo.

Tangu hapo klabu hizo hadi sasa hazijafanikiwa kutamba katika Ligi hiyo, japokuwa United inaweza kutamba kutokana kutawala kulibeba taji hiyo mara nyingi kuliko klabu yoyote nchini England tangu mwaka 1992, ambapo United imechukua mara 13 huku City ikichukua mara 2.

Lakini katika mara mbili hizi ambazo City wamechukua taji hilo, kuna wachezaji ambao walikuwa na mchango mkubwa katika chachu ya mafanikio hayo.

Kwa wachezaji ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwa timu hiyo hauwezi kuliacha jina la Yaya Toure, Vincent Kompany na Joe Hart.

Hawa ni baadhi ya wachezaji ambao walionesha umoja wao wa kuipigania klabu ya Manchester City na kufanikiwa kutwaa ubingwa lakini kwa sasa wanaonekana hawana nafasi katika kikosi hicho chini ya kocha mpya Pep Guardiola.

Yaya Toure

Ni nyota ambaye anaitumikia klabu hiyo katika safu ya kiungo, amefanya makubwa katika klabu hiyo tangu alipojiunga mwaka 2010 akitokea klabu ya Barcelona.

Kuondoka kwake katika klabu ya Barcelona kulitokana na madai kwamba alikuwa hana uhusiano mzuri na kocha wake Pep Guardiola ambaye alikuwa anakinoa kikosi hicho tangu mwaka 2008 kabla ya kuondoka mwaka 2012.

Toure alijiunga na Man City na kutoa mchango mkubwa sana hasa katika safu ya kiungo, wataalamu wanadai kuwa mchezaji huyo alikuwa na uwezo wa kupiga pasi za mwisho, kumilika mpira na kuhamasisha wachezaji.

Lakini ujio wa kocha Pep Guardiola katika kikosi hicho kunaonesha wazi kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 hana nafasi tena.

Joe Hart

Katika walinda mlango wa klabu hiyo, Joe Hart amekuwa na mchango mkubwa na alifanikiwa kuipa ubingwa, lakini pia ujio wa Guardiola kunamfanya mchezaji huyo akose nafasi ndani.

Guardiola alisema kwamba alikuwa hana mpango na mchezaji huyo tangu alipoambiwa kuwa anachukua nafasi ya kocha Manuel Pellegrin.

Hivyo mchezaji huyo hadi sasa tayari amewaaga wachezaji wenzake na mashabiki baada ya kucheza mchezo mmoja msimu huu katika michezo ya mitatu ya Ligi ambayo klabu hiyo imeshuka dimbani.

Mashabiki wa klabu hiyo wameshtushwa na mipango ya kocha huyo kumuacha mchezaji huyo japokuwa tayari klabu hiyo imemalizana na mlinda mlango wa Barcelona, Claudio Bravo kwa mkataba wa pauni milioni 15.4.

Vincent Kompany

Naye katika idara ya ulinzi mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa wa mafanikio ya klabu hiyo, lakini kwa sasa thamani yake inaonekana kuanza kushuka hasa kutokana kuwa na majeruhi ya mara kwa mara.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, japokuwa amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, ila kocha huyo amedai kuwa atamtumia katika michezo yake ijayo.

Beki hiyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji alishindwa kuisaidia timu hiyo ya taifa katika michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa kutokana na kuwa majeruhi.

Kompany alijiunga na timu hiyo tangu mwaka 2008 na ameisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili katika msimu wa 2011/2012 pamoja na 2013/2014.

Kwa upande wa kocha Guardiola inasemekana kuwa kocha huyo amekuwa akigombana na wachezaji wenye majina makubwa mara kwa mara kama vile nyota wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Ronaldinho, Deco na Samuel Eto’oo.

Mwaka 2008 kocha huyo aliweka wazi kuwa kikosi cha Barcelona kina wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini katika upande wake hana mpango na nyota wa klabu hiyo ambao ni Ronaldinho, Deco na Eto’oo.

Iliwashangaza wengi hasa kwa kumuacha Ronaldinho ambaye alikuwa na jina kubwa katika ulimwengu wa soka, lakini yeye aliweza kufanya hivyo na ndivyo inavyoweza kutokea katika klabu ya Manchester City kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles