31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Nkurunziza aanza jaribio la kutawala maisha Burundi

Pierre Nkurunziza
Pierre Nkurunziza

BUJUMBURA, BURUNDI

WAKATI hali ya utulivu ikielekea kurejea kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyotokana na uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu, mjadala wa kuondoa mihula ya urais unatarajia kuanza wakati wowote.

Iwapo hilo litatokea, Burundi itaungana na Uganda na Rwanda, mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyoondoa ukomo wa urais uliowawezesha marais wake Yoweri Museveni na Paul Kagame kubaki madarakani bila ukomo.

Mjadala huo uko njiani baada ya tume iliyoanzishwa na Rais Nkurunziza mwaka jana kuangalia mustakabali wa kisiasa wa taifa hilo, kukamilisha kazi ikisubiri kuwasilishwa bungeni kujadiliwa.

Tume hiyo ilisema kwamba sehemu kubwa ya mawazo iliyokusanya yalipendelea kuondoshwa kwa mihula miwili ya urais.

“Zaidi ya theluthi mbili ya watu ilitaka kuondolewa kwa ukomo wa urais. Inamaanisha kwamba rais anaweza kutawala kwa mihula mingi akipenda iwapo atachaguliwa na watu,” alisema mwenyekiti wa tume hiyo, Justin Nzoyisaba.

Alisema hilo litalazimisha kupitiwa upya kwa makubaliano ya Arusha na katiba ya nchi ambayo inakataza rais kugombea kwa muhula wa tatu.

Nkurunziza alizua utata wakati alipotangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu Aprili mwaka jana, akiitisha uchaguzi na kushinda miezi minne baadaye.

Hiyo ilitokea baada ya Mahakama ya Juu kudai muhula wake wa kwanza hauguswi na katiba kwa vile aliteuliwa kupitia makubaliano ya wabunge chini ya Mkataba wa Arusha 2005 uliolenga kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Tume hiyo yenye wajumbe 15 wakiwamo viongozi watatu wa dini, watatu wa kisiasa na wawakilishi wawili wa asasi za kiraia, itawasilisha ripoti bungeni na uamuzi wa mwisho ukitarajia kutolewa na Rais Nkurunziza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles