26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mgeja ataka Jaji Mutungi, Dk. Mwakyembe wajiuzulu

Dk. Harrison Mwakyembe
Dk. Harrison Mwakyembe

NA TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Tanzania Mzalendo Foundation, Hamisi  Mgeja amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi   na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, wajiuzulu kwa kile alichodai kuwa wameshindwa kumshauri Rais John Magufuli katika masuala yanayohusu Katiba na Sheria.

Mgeja pia amepinga kauli ya Rais Magufuli kutaka kupiga mnada majengo ya serikali baada ya kuhamia Dodoma.

Akizungumza   Dar es Salaam jana, Mgeja alisema watu hao wameshindwa kuzitumikia vema nyadhifa zao kumshauri Rais katika masuala ya Katiba na Sheria na kusababisha mvutano mkubwa unaochagizwa na kuvunjwa kwa haki za katiba za vyama vya siasa kufanya shughuli zao.

Alisema ingawa watu hao ni wasomi waliobobea katika masuala ya Sheria na Katiba lakini wameshindwa kutekeleza wajibu wao.

“Kama wamemshauri Rais kuhusu masuala ya Katiba na Sheria ambayo yamesababisha mvutano katika jamii naye hakuwakubalia basi niwaombe wawe waungwana wajiuzulu kulinda heshima zao,” alisema Mgeja.

Mgeja aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Shinyanga kabla ya kuhamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alisema jambo hilo si geni kwa kuwa hata wakati wa awamu ya kwanza, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Edwin Mtei alijiuzulu baada ya kukataliwa ushauri wake na rais wa wakati huo, Mwalimu   Nyerere kuhusu masuala ya IMF.

“Viongozi hawa walikuwapo tangu serikali zilizopita na wanajua sababu ya kuacha kuzuia shughuli za  siasa lakini wameshindwa kutumia uzoefu wao kumsaidia Rais, lolote litakalotokea baya watakuwa wameshiriki,” alisema Mgeja.

Alisema kukaa kimya kwa viongozi hao katika kipindi hiki ambacho nchi inakabiliwa na kukiukwa  katiba na sheria mbalimbali, hawawatendei haki wananchi licha ya dhamana waliyopewa na Rais.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles