31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli, Lowassa waibua mjadala

IMG-20160827-WA0022

NaVeronica Romwald, Dar es Salaam

KITENDO cha kusalimia kwa kushikana mikono kilichofanywa na Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa, kimeibua mjadala mzito.

Viongozi hao waliopambana vikali katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, walikutana  kwa mara ya kwanza juzi katika hafla ya Jubilei ya Dhahabu ya miaka 50 ya ndoa ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa na mkewe Anna.

Hafla hiyo ilifanyika katika  Kanisa la Mtakatifu Peter, Oysterbay, Dar es Salaam ambako viongozi mbalimbali walialikwa.

Kutokana  na tofauti za msimamo ya vyama vyao, Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliko Rais Magufuli na kile cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliko Lowassa  hivi sasa baada ya kujiengua CCM, watu wengi hawakutarajia kitendo hicho.

Lowassa alihama CCM na kwenda Chadema kwa kile alichoeleza kuwa ni kutoridhishwa na mchakato wa kumteua mgombea wa nafasi ya urais, huku Rais. Magufuli akiteuliwa wakati huo kuwania urais.

Siku kadhaa zilizopita, Chadema kilitangaza kufanya operesheni kubwa kiliyoipa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) ambayo itaambatana na maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia Septemba mosi.

Hata hivyo,  Serikali imepiga marufuku maandamano kupitia jeshi la polisi.

Wakizungumza na MTANZANIA jana kwa nyakati tofauti, baadhi ya wasomi na wanazuoni  walipongeza kitendo kilichofanywa na viongozi hao kwamba kimeonyesha ukomavu wa siasa, huku wakiamini huenda ni hatua nzuri ya kufikia mwafaka.

SEMBOJA

Mtaalam wa Masuala ya Uchumi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Profesa Joseph Semboja alisema kitendo kilichofanywa na viongozi hao kimemfurahisha mno  kwa vile  kimeionyesha dunia kuwa Watanzania ni watu wenye amani na upendo.

Alisema hatua hiyo  imeonyesha Watanzania wanaweza kuwa na tofauti, wakaendelea kuishi pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya jamii kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa lao.

Profesa Semboja aliwataka wananchi kujifunza kutokana na kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao.

Alisema si vizuri kutumia mfumo wa jino kwa jino  kwa vile  utaratibu huo ndiyo unaoweza kusababisha kukua zaidi   migogoro na wakati mwingine unasababisha umaskini kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwa sababu  muda mwingi wananchi hawana muda wa kushiriki katika shughuli za maendeleo kutokana na migogoro.

WANGWE

Profesa Samwel Wangwe alisema hatua hiyo ni ishara kwa Watanzania ambao wanapaswa kujifunza kuwa mazungumzo yana nafasi kubwa ya kuleta  muafaka katika mgogoro wowote kuliko kutunishiana misuli.

“Mazungumzo yana nguvu kubwa katika kuleta upatanishi katika migogoro mbalimbali inayotokea katika jamii kuliko kutumia njia nyingine ambazo zinaweza kusababisha vurugu na uharibifu wa mali za watu na upotevu wa maisha ya watu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles