23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kisiwa kinachoelea Ziwa Victoria kilivyozua taharuki Uganda

Wapishi wakishangaa kisiwa kikitia nanga katika ufukwe wa Munyonyo nchini Uganda.
Wapishi wakishangaa kisiwa kikitia nanga katika ufukwe wa Munyonyo nchini Uganda. PICHA NDOGO: Miongoni mwa wakazi wa kisiwa kinachoelea, ambao wengi ni wasanii wa muziki, uchoraji na sanaa nyingine.

NA JOSEPH HIZA,

NUSU ya kwanza ya Juni mwaka huu nchini Uganda ilitawaliwa na taarifa za uwapo wa kisiwa cha ajabu kinachoelea katika Ziwa Victoria zikienda sambamba na picha zilizosambaa mitandaoni.

Moja ya picha hizo inaonesha wageni katika ufukwe wa Commonwealth and Speke Resort huko Munyonyo katika kitongoji cha Kampala wakishuhudia maajabu hayo.

Pengine ni kitu kilichotokea miaka milioni 180 iliyopita wakati ganda la dunia lilipokumbana na kinachoitwa miondoko ya tectonic mamilioni ya miaka iliyopita.

Wapishi na wafanyakazi waliacha kazi zao kushuhudia kisiwa hicho kikitia nanga kikiwa na wakazi wake wote kabla hakijagusana na ardhi ya ufukwe huo maarufu kwa sherehe za harusi na utalii wa ndani.

Tangu kiripotiwe, kisiwa hicho kimekuwa kikihama kutoka eneo moja hadi jingine hasa kati ya maneo ya kutia nanga ya Ggaba, Port Bell – Luzira na Miami Beach.

Hii si mara ya kwanza kwa tukio hilo kuripotiwa. Na kwa mujibu ya wataalamu wa mazingira litaendelea kutokea kwa kadiri ya Ziwa Victoria linavyoishi na hali zinazowezesha ardhi kuachama na kisha kuelea.

Hali hiyo imeelezwa na walioshuhudia wakiwamo waandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ni kwamba ilikuwa ikiendelea hivyo kwa miezi minne.

Wakati walipokifikia kisiwa hicho kitu cha kwanza walichokiona ni bendera ya Uganda ikipepea katika mlingoti.

Kwa mujibu wa mmoja wa wakazi wa kisiwa hicho, Labatin Mwiima mlingoti huo wa bendera unalenga kuelekeza pande halisi za kisiwa hicho wakati kinapohama na huamua umbali ambao kisiwa hicho chenye ukubwa wa ekali 20 kimetembea.

“Unaamka asubuhi na kukuta mazingira tofauti. Jioni moja tulienda kulala katika eneo la kutia nanga la Port-bell na tuliamka tukiwa Ggaba,” anasema.

Maeneo hayo mawili ya kutia nanga yameachana kwa umbali  wa dakika 20 kwa boti.

Wakati hilo likiwa halijathibitishwa bado, kisiwa hicho kimeonekana kikiwa katika maeneo matatu ya kutia nanga karibu na mji mkuu wa Kampala.

Wengi wa wakazi katika kisiwa hicho ni wasanii, wengine wakiwa wamekaribishwa na marafiki kwa muda, wengine wakiwa wakazi wa kudumu wakiishi katika vibanda vilivyoezekwa kwa makuti.

Kipo umbali mrefu kutika nchi nyingine ambazo zinachangia Ziwa Victoria yaani mataifa jirani ya Tanzania na Kenya.

Wenyeji wanasema hawana wazo kuwa kisiwa hicho kitakuja zama siku moja, kwa sababu kinapoelea hawahisi mtembeo huo.

Kiwango cha uhalisia kinachohusiana na matukio ya kuelea kwa visiwa katika Ziwa Victoria kimetawaliwa na imani za kishirikina zaidi.

Hata hivyo, sababu watu wamekiita kisiwa hiki Jaja Magezi, ambaye hujulikana kama mzimu mwenye uwezo wa uponyaji. Hilo linaleta mtazamo wa kishirikina, lakini pia likionesha namna wengi walivyo na hamu ya kupata jibu sahihi juu ya sababu ya kuelea huko.

Lakini pia wenyeji hukiita Miremba, neno linalomaanisha Kisiwa cha Amani.

Inasemekana msomi mmoja nchini humo aliishiwa neno wakati aliposikia kuhusu kisiwa hicho kinachoelea na kurudi kutia nanga katika eneo lake la asili.

Naam, ni tukio linalokanganya wengi kuishia kushika vichwa kwa mshangao, lakini kuna maelezo ya kitaalamu kuhusu hali hii.

Geoffrey Kamese kutoka Chama cha Wataalamu wa Mazingira Uganda, ambaye alikitembelea, ana nadharia kwanini kisiwa hiki kinaelea.

Anasema kunaweza kuwa na maji chini ya ardhi na kutokana na mvua nzito, mizizi ya mazao inaachia na kufanya ardhi kuelea.

“Inawezekana kutokana na mabadiliko yanatotokea katika hali yetu ya hewa, kiwango cha maji ziwani kinaongezeka na udongo kulegea,” anasema.

Lakini pia anatahadharisha, “Watu wanapaswa kuwa waangalifu na wasiendelee kulima kwa sababu inaweza kudhoofisha udongo na kuzama.”

Bustani nadhifu za mihogo, mahindi, maharagwe na hata migomba imenawili katika kisiwa hicho na kutengeneza uoto wa asili huku ndege wakionekana huko na huko.

Lakini pia tukija na tafiti nyingine za wataalamu, visiwa vinavyoelekea ziwani si kitu kipya.

Kiuhalisia, visiwa vilivyotengenezwa na binadamu vimetengenezwa kuelea ziwani kwa madhumuni tofauti.

Kwa mfano, katika Ziwa Titicaca nchini Peru, kuna visiwa vinavyoelea takribani 70.

Sayansi ya urejeshi wa maji baridi pia imeonekana kutengeneza mwendo wa kuelea kwa ardhi tope na au visiwa vya ikolojia, ambao huja kwa namna nyingi.

Hii na teknolojia, ambayo imekuwapo katika dunia ya Magharibi tangu katika miaka ya 1980, na inaenea kwa kasi kote duniani kurejesha mifumo ya asili ya maji baridi.

Kesi za  uwapo wa visiwa vinavyoelea zimeripotiwa katika dimbwi la karbonate kaskazini mashariki mwa Mexico.

Aidha, uchunguzi wa kuhama kwa samaki katika Ziwa Nyasa uliofanywa miaka zaidi ya 30 iliyopita (rejea utafiti wa Oliver & McKaye. 1982. Floating Islands: A Means of Fish Dispersal in Lake Malawi, Africa. Copeia 1982 (2): 748-754).

Kazi hiyo ya kitafiti inaeleza ishara ya asili ya tungamo katika ziwa hilo. Uchunguzi uliofanyika katika miaka ya 1940 unaonesha uwapo wa tungamo zinazoelea zilizotokana na tope zilizozunguka Ziwa Nyasa, ambazo huachama kutokana na upepo na mawimbi.

Kwa sababu hiyo, haishangazi kushuhudia wakati wa misimu ya mvua, hali ya kibichi inapodhoofisha ardhi tope zenye uoto na udongo.

Tungamo kama hizo zinazoelea zimeripotiwa kila mahali kama vile katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Kufahamu asili ya visiwa vinavyoelea tunatakiwa kufahamu namba vilivyotokea. Zinatambuliwa na udongo hai, ambao unatofautiana kwa kina kuanzia nchi chache na koloni la mimea ya majini na wakati mwingine mimea ya nyanda za juu.

Hilo linaonesha mimea hiyo ni ya majini kiasili na huundwa kwa njia tofauti, baadhi ambazo ni pamoja na visiwa vinavyoelea, ambavyo ni kawaida katika maziwa yenye viwango vya maji vinavyotofautiana msimu kwa msimu.

Wakati wa mawimbi ya kiwango cha chini, mimea iliyopo ufukweni mwa ziwa hujikuta katika udongo wa asili na kuunganisha mizizi kuzunguka udongo na kutengeneza jamvi zito na imara.

Wakati viwango vya maji vinapoongezeka, mimea huvuta malighafi nyingi za udongo na hivyo kusababisha kuelea kwa tungano lenye udongo na mimea.

Hiyo ni aina ya tungamo zinazoelea zinazotengenezwa katika maziwa, ambayo yameathirika na ukame wa muda mrefu.

Linapokuja suala la visiwa vinavyoelea katika Ziwa Victoria, kama inavyojulikana ziwa hilo ni la maji baridi, ambalo sehemu kubwa yametokana na mvua.

Kwa miaka mingi tope zimetengeneza koloni la kingo zake za pwani kuumba jamvi linalohuisha mizizi ndani ya udongo wa asili kuelekea juu.

Inafahamika kwamba kiwango cha maji hupungua sana wakati ukame unapokumba eneo hilo.

Hilo pia liliwahi kutokea katika bwawa la nguvu ya umeme la Kiira nchini Uganda lililojengwa karibu na mlango wa ziwa hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles