27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Muhimbili kununua helikopta ya wagonjwa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida, wakikata utepe kuzindua magari mawili ya kusafirisha wagonjwa yaliyotolewa na ubalozi huo kwa ajili ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam jana.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida, wakikata utepe kuzindua magari mawili ya kusafirisha wagonjwa yaliyotolewa na ubalozi huo kwa ajili ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam jana.

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam.

BODI mpya ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetangaza mkakati wake wa kununua helkopta  maalumu itakayokuwa inasafirisha wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali nchini hadi hospitalini hapo.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk. Joseph Komwihangiro aliweka wazi nia hiyo jana mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Waziri alikuwa akizindua bodi hiyo na kupokea magari matatu ya kubebea wagonjwa zilizotolewa na Ubalozi wa Japan nchini.

“Kwa muda mrefu MNH imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo uhaba wa wataalamu, vitendea kazi na kukosa fedha za kujiendesha, tutahakikisha tunajifunza kwa wenzetu waliopita wapi walikuwa wakikwama ili tujinasue kutoka hapo.

“Ukweli tunatamani kuipeleka hospitalki hii mbele kwa kuboresha huduma za ubingwa, tumepokea magari hayo tunashukuru lakini tunapenda MNH iwe na angalau helkopta maana kumsafirisha mgonjwa kutoka Katavi kwa mfano hadi Muhimbili, ni changamoto kubwa,” alisema.

Akizungumza, Waziri Ummy alisema wazo hilo ni zuri kwa vile huduma za msaada wa dharura nchini bado ni changamoto kubwa.

“Tanzania mtu anaweza kufa akiwa njiani kwenda hospitalini, tukiziboresha huduma hizi ni wazi kwamba tutaweza kuokoa maisha ya watu wengi na ulemavu.

“Ni vema pia bodi mkakaa chini na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) mkaandaa mtaala maalumu wa kufundisha wataalamu wa huduma hii ya dharura.

“Nasema hivyo kwa sababu wapo wachache… mkakati wa serikali ni kupeleka ‘ambulance’ katika kila kata lakini changamoto iliyopo ni kuwa hatuna wataaamu wa kutosha,” alisema Ummy.

Naye Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida alisema ubalozi huo upo tayari kuendelea kushirikiana na serikali katika kuiboresha sekta hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles