33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rais wa Ufilipino atishia kujitenga na Umoja wa Mataifa

philippines-duterte
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte

 

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, ametishia kujitenga na Umoja wa Mataifa ikiwa wataiita vita yake dhidi ya madawa yakulevya  kuwa ni ile inayoenda kinyume na sheria za kimataifa.

Tishio hilo amelitoa ikiwa ni moja ya namna alivyojidhatiti kufanya mapambano makali dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya nchini Ufilipino.

Lakini pia kauli hiyo iliendana na amrisho lake katika mapambano dhidi ya dawa hizo ambapo aliwaamuru wananchi wake kuwapiga risasi wauza unga ambao watakataa kuwekwa chini ya ulinzi.

Pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa sheria itawaunga mkono askari watakao ua kwa kujihami wakati wa mapambano kati yao na watuhumiwa wa dawa hizo.

Rais Duterte alishinda urais huku akibebwa na sera yake madhubuti yakupambana vilivyo na matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ronald dela Rosa amesema zaidi ya watu 1,900 wameuwawa ndani ya wiki saba zilizopita katika harakati zakupambana na matumizi ya dawa za kulevya.

Ronald aliongea hayo alipokuwa akitoa ripoti ya vifo mbalimbali vilivyotokea tangu Rodrigo Duterte awe Rais.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles