31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TDL yaimarisha kilimo cha zabibu Dodoma

ZABIBUU

Na ARODIA PETER, aliyekuwa DODOMA

HISTORIA ya zao la zabibu mkoani Dodoma inaanzia mbali tangu utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo

wakati huo mazao karibu yote ya biashara yaliratibiwa kupitia vyama vya msingi.

Baadaye utaratibu huo ulibadilika baada ya Serikali kuanza kuuza mashirika yake ambayo mengi yalikuwa yakihusika moja kwa moja na mazao hayo kutoka kwa wakulima jambo ambalo lilichangia vyama vya msingi kuyumba na vingine kufilisika kabisa.

Kwa muda mrefu wakulima wa zabibu mkoani Dodoma wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kiasi kwamba licha ya kufanya kazi za kilimo waliendelea kukabiliwa na tatizo la kutopata faida na kubaki katika hali duni za umasikini.

Mmoja wa wakazi na mkulima wa zabibu katika Kijiji cha Handala mkoani Dodoma, Yarendi Makuya anasema

suala la kupata mahitaji muhimu, ujenzi wa nyumba bora pamoja na kusomesha watoto lilikuwa ni ndoto.

Hata hivyo kutokana na kuongezeka kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda hivyo hivi karibuni, wakulima wa zabibu wameanza kupata ahueni ya maisha baada ya wanunuzi kuwafuata hadi vijijini kununua zabibu.

Anasema katika siku za karibuni wanunuzi wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku hali inayotia matumaini kuwa kilimo cha zao hilo kina fursa ya kuchangia uchumi na kuinua maisha ya wakulima iwapo watawezeshwa ipasavyo.

Yarendi aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya wenzake alieleza kuwa hivi sasa baadhi ya kampuni zilizowekeza kwenye viwanda  zimeanza kujenga ukaribu na kushirikiana na wakulima ili yaweze kupata malighafi kwa ajili ya viwanda na hivyo kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Moja ya kampuni ambayo hivi sasa imejikita katika kilimo shirikishi na wakulima wa zabibu ni Tanzania Distilleris Limited ambao ni watengenezaji na wazalishi wa kinywaji cha konyagi na bidhaa zake (TDL).

TDL ambayo inamilikiwa na Kampuni ya TBL Group hivi sasa inashirikiana na wakulima kwa lengo la kuwawezesha  kuongeza uzalishaji wa zabibu.

Wakati wa msimu wa zabibu TDL kwa kushirikiana na wakulima hununua mazao hayo kwa bei nzuri na malipo kufanyika bila urasimu kama ilivyokuwa awali kupitia vituo vya ushirika na walanguzi wa mazao ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa wakiwapunja  katika bei.

“Katika miaka  ya karibuni tangu tuanze kufanya kilimo kwa kushirikiana na TDL tumeanza kupata mafanikio hasa ya uwezeshwaji katika kilimo kwa kupatiwa pembejeo,mbegu,madawa ya kuua wadudu,ushauri wa kitaalamu.

“Mbali na uhakika wa soko, kitu kingine tunachokiona kama muujiza kwetu ni kampuni kusaidia kusomesha watoto wa wakulima kupitia mfuko unaojulikana kama Zabibu Kwanza” anasema mkulima mwingine wa zabinu Mery Chizoza.

Mwanamke huyo anasema kuwa hadi sasa motto wake aitwaye Paschal Chizoza ameweza kuhitimu kidato cha nne kutokana na msaada wa TDL.

Mkulima mwingine Yohana Petro kutoka Kijiji cha Mpunguzi anauelezea ushirikiano wa wakulima wa zabibu na TDL kuwa ni pamoja na kusaidia watoto  wao kwa kuwapatia mahitaji ya elimu na kuwapunguzia mzigo wazazi.

“Watoto wamekuwa wakisaidiwa kulipiwa ada na kampuni imekuwa ikitoa misaada ya vitabu, daftari, sare za shule na kutupunguzia makali ya maisha  sisi wakulima kwa kuwa hali zetu za maisha ni ngumu” alisema Petro.

Hata hivyo mkulima huyo anajivunia kuona zabibu wanayozalisha ndiyo inatoa mvinyo unayopendwa zaidi na watu wa kiwango cha kimataifa licha ya kwamba wao hawana uwezi kununua kinywaji hicho baada ya kutoka viwandani.

Mtafiti wa mazao kutoka Kituo cha utafiti wa   Kilimo cha  Makutupora Viticulture Training and Research Center (MVTRC), Reon Mrosso anasema kuwa  wanaendelea kutafiti utafiti wa zao la zabibu ili kuwezesha uzalishaji  kuongezeka.

Mrosso anapongeza

“Naipongeza  juhudi za kampuni binafsi ikiwamo TDL kwa  kuwezesha wakulima kwa kuwapatia  mbegu na pembejeo za kilimo kwa sababu wakulima wetu wengi ni masikini na vipato vya ni duni, bila kuwezeshwa hawawezi kumudu gharama zote

Naye Meneja wa ubora wa Vinywaji vya Mvinyo wa TDL, Jackob Mwavika anasema bado kuna fursa kubwa ya kuzalisha zabibu kutokana na kuwapo ardhi na hali ya hewa inaofaa kwa kilimo cha zao hilo.

Mwavika anasema TBL Group tayari imeanza mkakati wa kushirikiana na wakulima na wadau mbalimbali ili kuendeleza zao hilo kupitia mpango wa kilimo shirikishi. Kupitia kilimo hicho wakulima watapatiwa pembejeo, mbegu bora kutoka Afrika Kusini pamoja na ushauri wa kitaalam.

“Ongezeko la matumizi ya mbegu bora ni moja  kati ya vitu vinavyohitajika kuwezesha kufikia uzalishaji na kukua kwa uchumi, kupunguza umaskini na kufikia lengo la kuwa na mazao ya kutosha na kuwezesha wakulima kupata mapato mazuri ya kuwawezesha kukidhi mahitaji yao na familia zao za kupanua shughuli zao za kilimo”anasema Mwavika.

Katika kutekeleza suala hilo, kampuni inaendelea kukamilisha mchakato wa kupata vibali vya kuingiza mbegu kwa mujibu wa utaratibu unaotakiwa.

Aidha Mwavika anaeleza kuwa zaidi ya wakulima  700 wa zabibu mkoani Dodoma na chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana MVTRC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles