27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ilala nao wabaini wanafunzi hewa 512

Sophia Mjema
Sophia Mjema

Na HADIA KHAMIS- DAR ES SALAAM

MAOFISA elimu na walimu wakuu wa shule za msingi za Manispaa ya Ilala, wametakiwa kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kina kwa kila shule ili kujiridhisha kama hakuna wanafunzi hewa.

Akitoa agizo hilo Dar es Salaam jana, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, alisema katika uchunguzi wa awali waliofanya katika shule za msingi 117 za wilaya hiyo, walizibaini sita kati ya hizo zina wanafunzi hewa 596 ambao tayari walikuwa wanapewa ruzuku ya fedha za Rais Dk. John Magufuli zilizoanza kutolewa tangu Januari, mwaka huu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya elimu bure.

Alisema bado hajaridhishwa na idadi hiyo ya wanafunzi hewa na aliwataka walimu wakuu wa shule za msingi kufanya uchunguzi wa kina na kujua sababu ya wanafunzi ambao hawafiki wasije wakawa sehemu ya wanafunzi hewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles