25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mwandishi kortini kwa kumchinja dada yake

BN-IX107_gavel_G_20150612161941

NA HAMIDU ABDALLAH (DSJ), DAR ES SALAAM

MWANDISHI wa habari wa kituo cha televisheni cha East Africa (EATV), Richard Steven na kaka zake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumchinja hadi kufa dada yao aliyetajwa kwa jina la Celina Bugaisa.

Steven na kaka zake, Robert Bugaisa (49) na Godfrey Stephen (39), wanatuhumiwa kutenda kosa hilo Julai 26, mwaka huu katika Mtaa wa Wazo Hill, Dar es Salaam.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Anipha Mngwira, wakili wa upande wa Jamhuri, Doroth Massawe, alidai washtakiwa walitenda kosa hilo huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria.

Hakimu Anipha alisema mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shtaka hilo hivyo kesi yao itatajwa tena Agosti 26, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles