23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wavulana wavua, wavaa sketi shule

_90488141_img-20160721-wa0006

LONDO, UINGEREZA

SHULE ya Longhill iliyoko Sussex, Uingereza imewatimua wavulana waliovalia sketi waliokuwa wanapinga kuadhibiwa baada ya kuvaa kaptula.

Wanafunzi hao wa darasa la tisa katika shule hiyo ni miongoni mwa wanafunzi 20 wavulana waliovaa kaptula za mazoezi badala ya suruali ndefu.

Uamuzi huo wa kuwatimua na kuwatenga baadhi yao umekuja kutokana na utovu wa nidhamu ulioonyeshwa na wanafunzi hao, huku baadhi yao wakitengwa hadi siku iliyofuata. Waliokubali kuvua kaptula hizo na kuvaa suruali ndefu hawakuadhibiwa.

Wanafunzi hao walikiuka taratibu badala ya kuvaa sare kamili wakati wa masomo kama walivyokuwa wameagizwa.

Wanafunzi watatu kati yao waliambia wavue sketi hizo lakini wote kwa pamoja walikataa.

Mwalimu Mkuu, Kate Williams, aliwaambia wanaweza kuvalia mavazi yoyote ili mradi yawe ni sehemu ya sare iliyokubalika shuleni.

Uamuzi uliofanywa na wavulana hao unatajwa kuwafungua macho watu wengi wakiwamo wazazi mara baada ya kuvaa sketi hizo za kuazima.

Mmoja kati ya vijana hao, Tyrone Evelyn (15), amesema kuwa wataendelea na kampeni ya kudai mabadiliko kutokana na hali mbaya ya joto iliyopo sasa.

“Hii ni sahihi kwa hali ya hewa, hatutaki kusikia joto na kusumbuka, kwa siku za hivi karibuni nimekuwa nikipata maumivu ya kichwa na ngozi kuwashwa kutokana na joto kali.

“Wasichana wanavaa sketi kwa hiyo sioni kwanini na sisi tusivae sketi, hivyo haya kwetu ni maandamano sahihi,” anasema Tyrone.

Tyrone na rafiki zake walivaa suruali wakiwa wanakwenda shule huku wakiwa wamezificha sketi kwenye mabegi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles