31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge aliyejiunga al shabaab ajilipua Somalia na kuua 13

Salah Nuh Ismail
Salah Nuh Ismail

Mogadishu:  Somalia

ALIYEKUWA mbunge   Somalia, Salah Nuh Ismail (57) ametajwa kuwa mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga katika shambulio lililoua watu 13 mjini Mogadishu.

Mbunge huyo aliyekuwa anajulikana kwa jina la Badbaado, alijiunga na bunge la Somalia mwaka 2009 akiwa mmoja wa wabunge 275 waliochaguliwa na rais wa zamani, Sheikh Sharif Ahmed.

Alijiuzulu mwaka 2010 na kujiunga na al-Shabab baada ya kuwaita wabunge wenzake “makafiri”.

Katika tukio hilo kundi la ugaidi la Al Shabab limekiri kuhusika katika milipuko miwili ilitokea karibu na kambi ya vikosi vya Umoja wa Afrika (AU).

Al-Shabab wamekuwa wakikabiliana na serikali ya Somalia ambayo inaungwa mkono na Umoja wa Afrika na jamii ya kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles