23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hillary mwanamke kwanza kuwania Ikulu Marekani

HILLARY Clinton
HILLARY Clinton

Washighton:  Marekani

HILLARY Clinton amekuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Marekani kuwania kiti cha urais baada ya kuidhinishwa rasmi kwenye mkutano mkuu wa chama cha Democrat.

Mgombea huyu atakuwa mwanamke wa kwanza kuiongoza nchi kubwa ya Marekani duniani kama rais kama atashinda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 8 mwaka huu.

Baada kuidhinishwa katika mkutano uliokumbwa na utata  kwenye ufunguzi, Clinton alipitishwa na wajumbe 2,382 ambao walihitajika ili apitishwe, kuwa mgombea rasmi wa Democrat dhidi ya Donald Trump wa Republican.

Mpinzani wake wakati wa mchujo, Seneta Bernie Sander,  alimuunga mkono na kumtangaza Hillary Clinton kuwa mgombea mteule kwa kauli moja ya kuwa mgombea rasmi wa Democrat katika mkutano mkuu uliofanyika Philadelphia.

Awali, wakati wa hotuba yake, Sanders alisema: “Hillary Clinton lazima awe rais ajaye wa Marekani”.

Clinton atapeperusha bendera ya chama hicho dhidi mteule wa Republican,Trump, katika uchaguzi  unaonekana kuwa mngumu katika historia ya Marekani.

Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton ambaye pia ni mume wa Hillary, alimsifu   mkewe akisema anafaa kuongoza taifa hilo.

Alimtaja Hillary kama “rafiki yangu mkubwa” na akasimulia walivyokutana na jinsi anavyojitolea katika utumishi wa umma.

Hillary Clinton aliuambia umati wa watu kuwa, “Siamini kwamba tumefanikiwa kuweka ufa mkubwa zaidi katika dari hili la kioo.

“Na iwapo kuna wasichana wadogo huko ambao hawajalala na wananitazama, ningependa kuwaambia, huenda nikawa rais wa kwanza mwanamke Marekani na mmoja wenu anaweza kunifuata,”  alisema Hillary.

Uteuzi wa Hillary ulikuwa hatua kubwa katika historia ya Marekani ya miaka 240. Nchini humo wanawake walipata haki ya kupiga kura mwaka 1920 baada ya marekebisho ya kifungu cha 19 cha  Katiba ya nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles