33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Diaspora sawa na mti wenye matunda unaopopolewa

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dorah Mmari Msechu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waishio Sweden walipokwenda kumtembelea ofisini kwake na kumkabidhi kikombe cha ushindi baada ya timu yao ya Kilimanjaro FC kubeba moja ya kombe la ligi ya Sweden.
Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dorah Mmari Msechu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waishio Sweden walipokwenda kumtembelea ofisini kwake na kumkabidhi kikombe cha ushindi baada ya timu yao ya Kilimanjaro FC kubeba moja ya kombe la ligi ya Sweden.

KUNA njia tano zinazofika eneo la Mburahati jijini Dar es Salaam, zinachukua muda tofauti kulingana na wingi wa magari barabarani, kama foleni ni kubwa. Inategemea pia wakati gani unatoka unakotoka na unatokea wapi. Kwa njia moja au nyingine utafika Mburahati.

Mburahati ni kama Ughaibuni

Baada ya kuishi miaka mingi Ughaibuni nimekuja kuelewa kwamba huu wakati wote naishi na mguu mmoja nyumbani Tanzania, sijahama hata siku moja labda kimwili lakini kiroho na kibinafsi  wakati wote moyo wangu ulikuwa nyumbani.

Kuna vitu vingi vidogo vidogo ambavyo sasa navielewa na ndio maana mizizi yangu haikuingia sana kwenye rutuba ya Ughaibuni kwani ndani ya nafsi yangu lazima nilielewa kwamba sitaweza kuwa na mizizi mirefu Ughaibuni kama sijakuwa nyumbani kwangu.

Sijui kama mnalielewa hilo au mnafahamu ninamaanisha nini. Bila ya kutengeneza kwenu wakati wote mtajisikia ni wageni hapo mlipo. Tengeneza kwenye shina muweze kuwa na amani ugenini na kwenye matawi.

Wakati wote ujue kwamba kwako hawatakutupa na kama moto ukiwaka hakikisha kwamba njia zote zinazokwenda na kutoka Mburahati zipo wazi kuokoa maisha na kurahisisha magari ya zimamaoto kuweza kuingia na kutoka.

Mshikamano wetu na kule tunakotoka usiwe ni wa kutoka upande mmoja tu ila nguvu ya mshikamano utoke pande zote na uwe wa aina tofauti unaokumbatiana na kunyongeana na kuwa kitu kimoja.

Sisi ambao tupo kwenye masoko tofauti ni wajibu wetu kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo, amabao wana uwezo wa kubuni na kutengeneza bidha kwa kuongeza thamani kwenye uzalishaji wa kawaida, wapate masoko pale tulipo. Tuchangie katika kufungua njia tofauti tuwawezeshe wenzetu wafike Mburahati na ujuzi na bidhaa zao.

Kuna umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya nyumbani na makazi yetu. Hatuzungumzii bidhaa tu ila pia habari, maelezo na hisia za masoko ya Ughaibuni.

Wajasiriamali wakiweza kuunganisha na masoko tofauti ya Ughaibuni hata kama ni madogo manufaa yake ni mengi. Mojawapo ni kuwawezesha wenzetu kupata huo ujuzi wa kuelewa masoko yanataka nini, ujuzi wa kutekeleza kwa haraka, wepesi na kwa urahisi matakwa ya walengwa na kuelewa mlolongo wote wa mawasiliano kwani kwenye uelewa na habari ni nguvu. Ukijua mwenzako anataka nini na habari ukapata mapema basi utajipanga vizuri.

Tanzania nchi yetu bado ni changa sana na muda wote tumekuwa ni soko la watumiaji, uzalishaji wa ndani wa kusitiri mahitaji yetu bado ni mdogo. Bidhaa nyingi zinatengenezwa sehemu mbali na soko ambalo pia inachangia katika kuongeza watu wengi na hasa vijana kutokuwa na ajira. Hali hii inaweza kubadilika kwa kuongeza ushirikiano zaidi na wana Diaspora, uwekezaji wa mazingira ambayo yanarahisisha huo uhusiano. Mara kwa mara unasikia kutoka sehemu tofauti nchini kwetu kwamba Wanaughaibuni sio watu wa kuaminika na tuna ajenda nyingine. Hii sio kweli kwani hakuna mtu ambaye atapenda nyumbani kwake kuharibikiwe.

Ukiangalia utaona wengi ambao tupo nje ya nchi tumeweza kufika sehemu nzuri tu ambapo kwa huo ujuzi tulionao ni moja ya hazina kubwa ambayo ikitumika vizuri Tanzania itaendelea kupiga hatua za kuwawezesha wengi kupata ajira haswa vijana.

Uhusiano kati ya jamii zetu za ughabuni na nyumbani ni mmoja wa misingi ambayo itatuwezesha nchi yetu kuchota ujuzi, uzoefu na kupata uwekezaji wa moja kwa moja au kupitia kampuni na mashirika tofauti. Hizi njia zote unafika Mburahati.

Mti wenye matunda ndio unaopopolewa, wanaughaibuni wanamatunda ambayo mengi yameiva kuliko kuyaachia kwenye mti tuyavune na kuhakikisha kwamba miti hiyo haiachi kuzaa.

Moja ya mifano mizuri ni jinsi Gazeti la Mtanzania imetoa hii nafasi na kukubali kushirikiana katika programu maalumu ya kuinua umuhimu wa Diaspora na kupanga na kweka mikakati ambayo itafungua milango na njia tofauti za kufika Mburahati. Mmoja wa waandishi wa gazeti hili atatembelea Ulaya Kaskazini kupata picha kamili ya jinsi Wanaughaibuni wanaishi na kupambana na mazingira hayo. Atatembelea Sweden, Norway, Denmark, Finland, Canada na hata Latvia na Litauen.

Ukishafahamu haya yote, basi iliyobaki ni kasi tu ya kutekeleza uliyoyalenga..

Tengo Kilumanga Email: [email protected] Tel: +467051263303  Twitter:@tengo_k

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles