23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais aagiza aliyefanya ngono na wasichana wadogo akamatwe

RAIS Peter Mutharika wa Malawi
RAIS Peter Mutharika wa Malawi

Lilongwe:  Malawi

RAIS Peter Mutharika wa Malawi amelitaka jeshi la polisi nchini humo kumkamata Eric Aniva kwa kujihusisha na tambiko la kusafirisha wasichana wadogo na kufanya nao ngono.

Alitoa agizo hilo kutokanana  taarifa zilizotolewa na Shirika la Utangazaji  la Uingereza (BBC) na kuenea dunia mzima.

Rais Mutharika alisema amechukizwa na yaliofichuliwa katika habari hiyo na ameapa kukabiliana na utamaduni wa aina hiyo.

“Nimeambiwa kuwa ukiukwaji na unyanyasaji huu unafanyika kwa kivuli cha utamaduni ambao mimi nimeona   haikubaliki,” alisema Mutharika katika taarifa yake.

Rais pia anataka polisi kuchunguza tukio hilo na kumshitaki mtuhumiwa kwa uovu huo ambao yeye tayari amekiri na watu wote waliohusika katika ukiukwaji wa haki za watoto wawaajibishwe.

Aniva ambaye pia ni muathiriki wa   Ukimwi anatoka kusini mwa nchi hiyo.

Mtuhumiwa huyo aliyepewa jina la utani la ‘fisi’ kwa   uovu huo atashtakiwa kwa kukiuka haki za watoto.

Aniva (40),  analipwa kwa kufanya ngono na wasichana wadogo na kuwatoa ubikira kama tambiko la kuwasafisha.

 

Mtuhumiwa huyo  aliripotiwa kufanya mapenzi na zaidi ya wasichana 100 na  kulipwa dola za  Marekani 3.9 hadi 6.6 kwa kila binti kwa kufanya nao mapenzi kwa siku tatu kila mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles