25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘Kukua kwenye umasikini kunanifanya niwe bingwa’

Mo Farah
Mo Farah

LONDON, ENGLAND

MWANARIADHA nchini England, Mo Farah, ameweka wazi kwamba, kuzaliwa na kukua katika mazingira ya umasikini kumemfanya awe bingwa katika michuano mbalimbali ya kukimbia  duniani.

Nyota huyo amedai alikuwa anaishi katika mazingira magumu tangu alipozaliwa mjini Mogadishu nchini Somalia, hivyo alitamani siku moja kuja kuwa tajiri ambaye angeweza kuwasaidia watu wa hali ya chini.

Farah anatarajia kushindana katika mashindano makubwa ya Olimpiki mwaka huu yanayotarajia kufanyika mwezi ujao mjini Rio de Janeiro nchini Brazil, hivyo amedai akikumbuka alikotoka anakuwa na nguvu ya kufanya vizuri.

Bingwa huyo mara mbili wa michuano ya Olimpiki, amewataka wanamichezo wasikate tamaa na hali duni ya maisha yao, wapambane ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Nimetokea kwenye maisha ya hali ya chini, ndugu zangu pamoja na watu walionizunguka walikuwa wanaishi katika maisha ya hali ya chini, hivyo hali hiyo ilinifanya nipambane ili niweze kuwasaidia.

“Ninaamini hali hiyo imenifanya niwe hapa kwa sasa, kila wakati nakumbuka nilikotoka na ndio maana napata mafanikio makubwa.

“Siku zote ili kutimiza malengo, lazima upambane, hakuna kisichowezekana, kwa mwanamichezo yeyote mwenye lengo la kutaka kufika mbali kwanza lazima aangalie alikotoka hasa kwa wale waliotokea katika maisha ya hali ya kawaida.

“Wapo ambao wanatoka kwenye maisha mazuri na bado wanafanya vizuri kwa kuwa wanajituma ili kutangaza jina,” alisema Farah

Farah amedai akikumbuka maisha yake ya utotoni anakuwa na hasira, kwa kuwa kuna wakati alikuwa anakosa chakula na hayo yalikuwa maisha ya kawaida kwake na aliyazoea.

“Maisha ni safari ndefu, nakumbuka wakati nina umri mdogo, ipo siku inapita kwa mlo mmoja na hali hiyo ilikuwa ya kawaida kwa kuwa niliizoea na siku zilikuwa zinaenda.

“Nilikuwa nalala chumba kimoja chenye watu nane, hali ambayo ni hatari katika maisha ya binadamu, lakini ukiangalia maisha ninayoishi sasa ni tofauti kabisa kwa kuwa nilijitambua na nikapambana vilivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles