31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatishia kuwakamata  wanaomshambulia Mugabe

Rais Robert Mugabe
Rais Robert Mugabe

HARARE: Zimbabwe

SERIKALI ya Zimbabwe imesema itawashughulikia maveterani wa vita vya ukombozi nchini humo, wanaompinga Rais Robert Mugabe na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Maveterani hao wanamwita    Mugabe kuwa dikteta na msaliti ambaye amekuwa akiendesha nchi kwa  ujanja ujanja   huku akiacha matatizo ya uchumi yakizidi kuwa mabaya.

Pia wanampiga mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe,ambaye anaoneka  kuwa nguvu kuliko  Mugabe mwenye umri wa miaka 92.

Serikali ya Zimbabwe  imekitaja kitendo cha maveterani hao  kama cha usaliti, ikisema itawachukulia hatua wote waliohusika.

Maveterani hao wanadai Ris Mugabe ni dikteka aliyeuangusha uchumi wa Zimbabwe.

Kabla ya matukio   ya sasa,  maveterani hao walikuwa wakimuunga mkono Mugabe kwa dhati tangu nchi hiyo ilipojinyakulia uhuru wake katika miaka ya 1970, na ndiyo waliomsaidia kushika   madaraka nchini humo.

Hata hivyo, hivi aasa wanasema hawatamuunga mkono Mugabe   ambaye anataka kuwania muhula mwingine wa urais mwaka  2018.

Limekuwapo  ongezeko la maandamano ya kupinga utawala wa Mugabe katika  siku za  karibuni   hasa kutokana na uchumi wa Zimbabwe kuendelea kodorora  na kufikia kiwango cha  serikali kushindwa kuwalipa mishahara wafanyikazi wake.

Chama cha Zimbabwe National Liberation War Veterans Association (ZNLWVA) kimemshutumu Mugabe kwa  rushwa   na matumizi mabaya ya fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles