28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni za kigeni zinavyoshindana kwenye mafuta, gesi Afrika

Maersk-Viking

Na FARAJA MASINDE,

UCHUMI wa Bara la Afrika unatajwa kukua kwa kasi zaidi katika kipindi cha miongo miwili ijayo, hali hiyo inatokana na ongezeko la watu, kukua kwa miji na kuibuka kwa tabaka la kati la uchumi likichagizwa na rasilimali zilizopo.

Kampuni zaidi ya 500 kutoka kwenye mataifa ambayo yanajihusisha na utafiti wa nishati hizo kwa sasa yamejikita zaidi kwenye nchi za Afrika.

Bara la Afrika linaelezwa kuwa awali lilikuwa na tani karibu milioni tisa za mapipa ya mafuta ambayo yalikuwa hayasafishwi, yanayozalishwa kila siku huku asilimia 80 yakitoka kwenye nchi za Nigeria, Algeria na Angola.

Taarifa kwa mijibu wa majarida mbalimbali duniani zinaweka wazi kuwa zaidi ya kampuni 500 kutoka Ulaya, Marekani na Asia zinashindana kwa kila mmoja kuwania haki ya kupata mikataba ya kufanya tafiti pamoja na uchimbaji wa mafuta na gesi barani Afrika.

Takwimu zinaonyesha kuwa, kuwapo au kugundulika kwa akiba kubwa ya mafuta na gesi Afrika kumevutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka Marekani, China na Ulaya.

Hata hivyo, si rasilimali za mafuta na gesi pekee, pia kuna vitu vingine ambavyo vimeongeza ushawishi na ushindani miongoni mwa kampuni hizo zikiwamo rasilimali za  madini ambzo zinafanya Afrika kwa sasa kukaa juu ya kilele katika nyanja ya uwekezaji kwenye mataifa ya Magharibi.

Kampuni nyingi za Magharibi ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikipewa nguvu na serikali za nchi zao zimefikia malengo yao ya kupata mikataba mizuri inayowapatia nafasi ya kufanya tafiti ikiwamo pia kuchimba nishati hizo za mafuta na gesi, msukumo huo pia umekuwa ukichangiwa na soko la uhakika licha ya kuporomoka kwa bei ya mafuta kwa siku za hivi karibuni katika soko la Dunia.

Ni dhahiri kuwa kumekuwapo na mafanikio makubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma kabla ya uhuru, ambapo nchi nyingi za Afrika zilikuwa zikitoka kwenye mikono ya wakoloni, kwa sasa mambo ni tofauti kwani nchi zenye rasilimali za mafuta na gesi mbali ya kuja na mikataba mizuri yenye manufaa lukuki kwa rasilimali hizo, pia zimeanzisha kampuni za ndani ambazo si tu zinashindana na kampuni za kigeni, bali pia zinapewa kipaumbele katika mikataba hiyo ili kuhakikisha uchumi wa taifa husika unaimalika.

Nchi kama Nigeria ni moja ya zile zinazotawala barani Afrika kwa uzalishaji wa mafuta, ambapo inatajwa kuwa na kampuni takriban 70 zinazojihusisha na utafiti pamoja na uchimbaji wa mafuta na gesi.

Nigeria ambayo ina ukubwa wa kilometa za mraba 924,000 likiwa na idadi kubwa zaidi ya watu Afrika (milioni 170.1) pamoja na Pato la Ndani la Taifa (GDP) Dola za Marekani 450.5 bilioni, linashika nafasi ya pili kwa kuwa na akiba iliyothibitishwa ya mafuta ambayo ni mapipa bilioni 37.2 likiwa pia linaongoza kwa kuwa na akiba ya gesi asilia iliyothibitishwa ya futi za ujazo trilioni 186.7.

Itaendelea wiki ijayo. Kwa maoni ushauri 0653045474.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles