25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm atamba kurudisha ubora wa Yanga

Pluijm

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM,
KOCHA mpya wa timu ya Yanga, Mholanzi Hans van Der Pluijm, ameeleza kuwa amerejea kwenye timu hiyo kurudisha ubora wa awali wa kikosi hicho aliouacha, huku akipanga kuendeleza falsafa yake ya soka la kushambulia.

Pluijm, aliyetua nchini majira ya saa 8.30 usiku wa kuamkia jana, amekuja kurithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo, aliyetimuliwa kuinoa Yanga juzi, ambapo sasa inakuwa mara yake ya pili kukinoa kikosi hicho baada ya kufanya hivyo msimu uliopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kutua nchini, Pluijm alifurahia kurejea tena kuwa kocha wa kikosi hicho, huku akidai alitarajia jambo hilo kutokea.

“Nimefurahi kurejea tena Yanga, jambo nililolitarajia, nilifanya kazi kubwa nikiwa hapa, hivyo nakuja kuendeleza pale nilipoishia,” alisema.

Akizungumzia falsafa anayokuja nayo, Pluijm alisema: “Nitaendeleza falsafa yangu ya kucheza soka la kushambulia, kwa sababu naamini kuwa ili ushinde, basi ni lazima ufunge mabao ya kutosha.”

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni jana jioni, Mholanzi huyo alikuwa hajasaini mkataba wa kukinoa kikosi hicho, lakini alivyotua jana alidai ana matumaini ya kumalizana na viongozi wa timu hiyo hadi kufikia leo.

Mholanzi huyo anatarajia kuinoa tena Yanga sambamba na msaidizi wake, Boniface Mkwasa, ambaye naye amerejeshwa, wawili hao mara baada ya kuondoka Yanga walipata dili nchini Saudi Arabia kuinoa Al Shoalah, ambayo walishindwa kudumu nayo kutokana na matatizo ya timu hiyo.

Pluijm hadi anamaliza mkataba wake wa miezi sita Juni, mwaka huu alifanikiwa kuiongoza Yanga kwenye michezo 19, huku akifanikiwa kushinda mechi 11, sare sita na kufungwa michezo miwili dhidi ya Al Ahly (1-0) na Mgambo JKT (2-1).

Nsajigwa asimamia mazoezi

Kwenye mazoezi ya jana asubuhi kocha msaidizi wa timu ya vijana ya Yanga, Shadrack Nsajigwa, ndiye aliyesimamia mazoezi hayo.

Baadhi ya matukio yaliyotokea ni aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Leonardo Neiva, kuzuiwa kuongoza mazoezi hayo na kubakia mtazamaji tu, huku baadaye akifuatwa na gari na Meneja wa timu, Hafidh Saleh aliyeambatana na Maximo.

Maximo alimchukua Neiva na kiungo mkabaji, Emerson de Oliveira na kuondoka nao kutokana na mikataba yao kusitishwa.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles