28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ukawa waitoa jasho CCM

untitledNa Waandishi Wetu, Dar na Mikoani UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeonekana kukitoa jasho Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika nchini kote jana. Licha ya kuwapo na mchuano mkali kati ya Ukawa na CCM, uchaguzi huo ulitawaliwa na dosari nyingi zilizosababisha uchaguzi usimamishwe katika maeneo kadhaa kutokana na vurugu au kukosekana vifaa vya kupigia kura. Mbali ya CCM, Chadema na CUF kuchuana vikali katika maeneo mbalimbali, Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) kimeibuka kwa kishindo mkoani Kigoma kwa kupata ushindi katika mitaa 10 kati ya 18 huku CCM ikipata mitaa 6 na Chadema mitaa miwili Katika Jimbo la Kigoma Kaskazini eneo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mwandiga, ACT- Tanzania imepata mitaa 8, CCM mitaa 4 huku ADC ikiambua mtaa mmoja. Chadema wang’ara Geita, Mwanza Mchuano katika Kata ya Igoma, umekuwa mkali ambapo CCM na Chadema waliweza kujizolea mitaa miwili kila mmoja. Chadema ilishinda mtaa wa Kanindo na Bukaga, huku mitaa ya Kishiri B na Mecco Mashariki CCM walishinda. Lakini katika kituo cha Kirumba shule ya Msingi, CCM waliongoza kwa kura 318 na Chadema walipata kura 249. Kata ya Katoro Geita, Chadema wameshinda vitongoji 16 na CCM wakiambulia kitongoji kimoja kati ya vitongoji 17. DAR ES SALAAM Jijini Dar es Salaam, matokeo yaliyotangazwa katika Mtaa wa Mkunduge Kata ya Tandale, mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Omari Kato kwa kupata kura 600 na kumshinda mpinzani wake, Tamimu Omari (CCM) ambaye alipata kura 409. Pamoja na hali hiyo , wagombea wa ujumbe wa Mtaa kutoka CUF wamefanikiwa kushinda katika uchaguzi huo. Mtaa wa Muhalitani, aliyeibuka na ushindi, ni Sudi Yussuph kwa kura 396 dhidi ya mpinzani wake, Jumanne Kidodo aliyepata kura 169. Mtaa wa Buguruni Malapa, Chama cha Wananchi (CUF), kilifanikiwa kutetea mtaa huo kwa Karim Malapa kupata kura 524, huku mpinzani wake wa karibu, Said Mwembe (CCM) akipata kura 381 na Ishak Nyota wa ADC alipata kura 193. Mtaa wa Maruzuku, mgombe wa CUF alikuwa akiongoza katika matokeo ya awali, huku katika mtaa wa Mbuyuni mgombea wa CUF, Mohamed Kassim alishinda kwa kura 858 dhidi ya Abdallah Aziz wa CCM aliyepata kura 694. Katika Mtaa wa Madenge, Adam Penza (CUF) alishinda kwa kupata kura 626 dhidi ya Minshehe Ndegeto (CCM) aliyepata 569 na Sharifa Msangi aliambulia kura 21. Geita wataka kura zichomwe moto Kutoka Geita, habari zinasema mpaka saa 1: 22 usiku kituo cha Manispaa kilikuwa kikiendelea na upigaji wa kura kutokana na karatasi za kupigia kura kumalizika na wananchi kusubiri nakala zingine za karatasi. Katika Mtaa wa Rwenge, kuliibuka vurugu kutokana na madai kuwa kura zilizokuwa zimepigwa zimechakachuliwa saa 10 jioni. Hali hiyo, ilimlazimu msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Margareth Nakainga, kuamua kuahirisha uchaguzi wa mtaa huo hadi Jumapili ijayo. Kwa mujibu wa wakazi wa mtaa huo, waliojiandikisha watu 1,195, lakini karatasi za kupigia kura zilikuwa 200. Musoma Katika kata ya Mwigobero Mtaa B, mgombea wa CCM Sidney Madenge alishinda pamoja na wajumbe wake wote hivyo mgombea wa Chadema, Deogratius Japani kuangushwa. Mtaa D wa Mwigobero, mgombea wa CCM, Mohamed Hussein alimshinda mgombea wa Chadema, Damian Manyonyi kwa kura 74 kwa 49. Katika Kata za Irongo na Mukendo wanachama wa CCM walionekana kushangilia ushindi mitaani, licha ya matokeo kutobandikwa na kutangazwa rasmi. TANGA Taarifa kutoka mkoani Tanga zinaeleza kuwa CUF, kimefanikiwa kushinda uenyekiti wa Mtaa wa Makoko kwa kupata kura 174 dhidi ya 78 za mgombea wa CCM. Taarifa kutoka wilayani Pangani, zinasema CUF imefanikiwa kushinda katika kijiji na vitongoji vinne katika Kata ya Pangani Mashariki, huku pia ikifanikiwa pia kuzoa vijiji na vitongoji katika Kata ya Mkwaja. Kata ya Abushiriki, Chadema imeshinda vitongoji viwili na katika Kata ya Mkaramo, CUF imeshinda katika vijiji viwili na vitongoji vyake. Kata ya Madanga, CUF imekishinda CCM kwa kupata ushindi katika vijiji na vitongoji vyote. MBEYA Mkoani Mbeya,Chadema kimefanikiwa kuongoza katika matokeo ya awali ambapo katika Kata ya Vwawa wilayani Mbozi, kilishinda vitongoji 28, huku CCM wakiambulia 17. Katika Wilaya Momba katika Mji mdogo wa Tunduma, CCM imefanikiwa kushinda kwa kupata viti 16, huku Chadema wakipata vitongoji 9 na katika Kata ya Momba Chadema imepata vitongoji 46 na CCM 16. Huko Wilaya ya Rungwe Kata ya Bagamoyo , CCM imefanikiwa kushinda vijiji vyote vine, huku kwa Wilaya ya Mbarali Kata ya Rujewa, CCM ikifanikiwa kupata ushindi wa vijiji na vitongoji 47 na Chadema ikipata viwili. Kwa upande wa Mbeya Vijijini, Kata ya Mbalizi, Chadema inaongoza kwa kupata saba, CCM ikiambulia kiti kimoja. Na Katika Kata ya Forest, Chadema ilifanikiwa kushinda mitaa yote saba. Kata ya Maendeleo Mbeya Mjini, CCM imengoza mitaa minne, huku Chadema wakiambulia mtaa mmoja ambapo katika Kata ya Majengo, CCM imeongoza kwa kupata vitongoji vyote. Mtaa wa Mbugani wilayani Mbozi , Chadema (227), CCM (160), Mtaa wa Masaki Chadema (99), CCM (44) Na wilayani Kyela, CCM imefanikiwa kushinda vijiji 25 na Chadema haikupata kitu. SONGEA Chadema kimepata ushindi wa mitaa sita katika matokeo ya awali. Mitaa ambayo imekwenda kwa Chadema, ni Mjini, Sabasaba, Mbulani, Namatuli, Nonganonga, Mwinyimkuu Moyo huku CCM ikichukua mitaa ya Majimaji, London,Namanyigu, Mfaranyaki B, ambapo mitaa mingine ilipita bila kupigwa katika manispaa hiyo yenye mitaa 90. UKEREWE Taarifa kutoka wilayani Ukerewe zinasema CCM, kimefanikiwa kushinda mitaa mitano kwa mujibu wa matokeo ya awali, huku Chadema ikiambulia kitongoji kimoja. Monduli Kitongoji Kambi ya Mkaa, Chadema (27) CCM (13),Mwanga mtaa wa Lwami,Chadema (55), CCM 35). Monduli Mto wa Mbu, Kijiji Jangwani, Chadema (147), CCM (124) Arumeru Magharibi, kitongoji cha Endulele,Chadema (170),CCM (130),Ushirombo Mjini,Chadema inaongoza vitongoji 10 na CCM vitongoji 4. Moshi Manispaa; Kitongoji Longuo A,Chadema (206),CCM (66), Ukonga Mtaa wa Kivule Majohe,Chadema (231),CCM (77) Musoma Vijijini, Kijiji cha Muhoji, Chadema (197),CCM (464). Ubungo, Mtaa wa Msewe, Chadema (683),CCM (356) Kinondoni, Mtaa wa Mwenge Nzasa,Chadema (344),CCM (318) TARIME Tarime Forodhani boda (kitongoji), Chadema (289), CCM (90) na Forodhani Kijiji, Chadema (312),CCM (99) Mwanga , Kitongoji Mgagao, Chadema (56),CCM (32) Rorya, Mtaa Ngasaro, Chadema (480), CCM (360) Arumeru Mashariki, Mtaa wa Manyata, Chadema (168), CCM (91). KILIMANJARO Kwa upande wa Wilaya ya Hai, eneo la Mji wa mdogo wa Hai, matokeo ya awali Chadema wanaongoza kwa vitongoji tisa ,huku CCM ikishinda vitongoji vinane kati ya vitongoji 17 Kitongoji Uzunguni, Chadema (120) mgombea wa CCM (70), kitongoji cha Kilima mbogo Chadema (35), CCM (117). Kitongoji wa Jiweni, CCM (58) ,Chadema (178), Kitongoji Kambi ya Raha, Chadema (289), CCM (108). Kitongoji Nyerere, Chadema (127),CCM (85), Kitongoji cha Amani, Chadema (93),CCM (75). Kitongoji Mlima Shabaha, Chadema (313),CCM (250),vitongoji Umoja Chadema (162), CCM (141) Kitongoji cha Bomani, Chadema(275) ,CCM (158), Gezaulole, Chadema (429),CCM (280), Kitongoji cha Kambi ya Nyuki, Chadema (54), CCM (148). KIFO Mkoani Mwanza, habari zinasema Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Hida Hassan alitanganza kusimamishwa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Sweya, Kata ya Luchelele wilayani Nyamagana baada ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Masome kufariki dunia ghafla jana mchana katika Hospitali ya Rufaa Bugando alikokuwa akipatiwa matibabu. Akizungumza na MTANZANIA jana, Hassan alisema hali ya Masome ilibadilika ghafla baada ya kufikishwa hospitalini hapo kwa matibabu. “Msome amefariki dunia kutokana na shinikizo la damu (BP), kwa hiyo kwa mamlaka niliyonayo nasimamisha uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti hadi nitakapotangaza tena,” alisema Hassan. ARUSHA Mkazi wa Kata ya Mbauda, jijini Arusha aliyetambulika kwa jina moja la Sele, amefariki dunia akiwa kwenye foleni ya kupigia kura. Mtu huyo alikuwa amejiandikisha kupiga kura katika kituo cha Mbauda kilichopo ofisi ya ofisa mtendaji wa Kata ya Sombetini. Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo walidai kwamba kijana huyo alidondoka ghafla saa 2.00 asubuhi akiwa kwenye foleni ambayo ilikuwa na msongamano mkubwa wa watu. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Joseph Lazaro, alisema kijana huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24 baada ya kuanguka alisaidiwa na wasamaria wema kituoni hapo ambao walimkimbiza hadi nyumbani kwao. “Taarifa tulizozipata hapa ni kwamba yule kijana aliyedondoka kwenye foleni amefariki dunia na anatarajiwa kuzikwa kesho (leo),” alisema Lazaro. Nako Sumbawanga mkoani Mbeya, habari zinasema hali ilichafuka baada ya kuzuka mtafaruku kutokana na kuchelewa vifaa vya uchaguzi, kitendo kilichosababisha kundi la wananchi hasa vijana wenye hasira kuchoma moto

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. nawashukuru kwa taarifa zenu nzuri na za wazi; ccm bado wanaishi kwa mazoea, lazima wang’oke 2015, ufisadi, uongo, wizi, ulaghai ndio marafiki zao. Tumechoka, wapishe chama kingine banaaa! Amani ya kweli haiji bila kuwa nahaki ya kweli kwani Amani ni zao la haki ya kweli…!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles