27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yaikabidhi Malaysia bawa la ndege iliyotoweka

Pg 2

NA TUNU NASSOR,

BAWA la ndege aina ya Boeing 777 linalodhaniwa kuwa ni la ndege ya Shirika la Malaysia Airlines yenye namba MH370, iliyotoweka Machi 8, mwaka juzi ikiwa na abiria 360 hatimaye limekabidhiwa kwa Serikali ya nchi hiyo.

Bawa hilo la kulia liliokotwa Juni, mwaka huu huko Kojani, Pemba na mvuvi, Chunguwa Hamadi Chunguwa na baada ya kuchunguzwa na wataalamu wa ajali za ndege nchini waligundua kuwa ni la ndege aina ya Boeng 777.

Baada ya kukabidhiwa kwa ujumbe wa kutoka Malaysia bawa hilo lilichukuliwa na kampuni ya kusafirisha mizigo ya DHL tayari kwa kusafirishwa kuelekea nchini Australia kwa uchunguzi zaidi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho, alisema Juni 20 mwaka huu walipata taarifa ya kuokotwa kwa bawa hilo la ndege kutoka Kojani na kutuma wataalamu kufanya uchunguzi.

Alisema baada ya uchunguzi wa kina waligundua kuwa ni la ndege kubwa na kwa kuwa Afrika Mashariki haijawahi kupata ajali kubwa hivyo walidhani moja kwa moja bawa hilo ni la ndege hiyo ya Malaysia.

“Hapa tunawakabidhi bawa lililookotwa na wavuvi  huko Kojani Pemba kwa ujumbe kutoka Malaysia unaoongozwa na Balozi wa Australia Afrika Mashariki, John Feakes, ambako ndiko uchunguzi zaidi utafanyika,” alisema Dk. Chamuriho.

Kwa upande wake Feakes, alisema kupatikana kwa bawa hilo kutawafariji ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo.

Naye Mkurugenzi Mwandamizi wa ajali za anga kutoka Malaysia, Aslam Basha Khan, alisema anashukuru  jitihada zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kuliokota na kulitunza bawa hilo.

“Kama mtaokota kipande kingine tunaomba mtutaarifu na tutatoa ushirikiano na msaada wa kiuchunguzi,” alisema.

Alisema bawa hilo ni kipande kikubwa zaidi ya vilivyowahi kuokotwa Mauritius, Msumbiji na Madagascar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles