24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania kujifunza ufugaji Rwanda

NG'OMBE

NA WALTER MGULUCHUMA, Mpanda

CHAMA cha Wafugaji Tanzania (CCWT)  mkoani Katavi, kinatarajia kuwapeleka  Rwanda  baadhi ya wanachama wao  wakajifunze ufugaji bora.

Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa   CCWT Mkoa wa Katavi, Mussa Kabushi alipozungumza kwenye kikao cha  wafugaji mkoani hapa.

Kikao hicho kilihusisha pia wenyeviti wa halmashauri na madiwani wa halmashauri hizo.

“Tatizo linalowakabili wafugaji wengi hapa nchini ni ukosefu wa elimu ya ufugaji bora wa kisasa. Kwa kulitambua hilo, sasa tumeamua kuwapeleka baadhi ya wanachama wetu  Rwanda wakajifunze ufugaji bora wa kisasa.

“Kilio kikubwa kwa wafugaji wa Mkoa wa  Katavi ni kutotengewa maeneo ya kufugia na hali hii imekuwa ikiwafanya baadhi ya wafugaji kufugia kwenye maeneo yasiyostahili na kusababisha   migogoro isyokuwa na maana.

“Kwa hiyo  tunaiomba Serikali ya mkoa wetu, ifanye kila linalowezekana  tupate maeneo hayo kwa ajili ya kuimarisha ufugaji wetu,” alisema Kabushi.

Naye Meya wa Manispaa ya Mpanda, Willy  Mbogo, aliviomba vijiji vyenye ardhi kubwa  vitenge maeneo ya wafugaji  kuondoa  migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Raphael  Kalinga, alisema Mkoa wa Katavi unakabiliwa na tatizo la wingi wa mifugo kwa kuwa wafugaji wengi wamekuwa wakiingia mkoani humo kutoka mikoa mingine nchini.

Aliwataka wafugaji waache  tabia ya kusafirisha mifugo na kuipeleka katika maeneo yasiyostahili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles