33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Gesi ya barafu yagundulika Tanzania

 

Helium-logo-large

Mwandishi Wetu na Mashirika ya Habari,

BAADA ya kugunduliwa kwa gesi asili mkoani Mtwara, sasa watafiti kutoka nchini Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu aina ya Helium.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalamu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu hapa nchini.

Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la Bonde la Ufa la Tanzania.

Ugunduzi huo ulitangazwa jana nchini Japani na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa likiwemo Shirika la Utangazaji la nchini Uingereza (BBC).

Katika taarifa hiyo ilielezwa kuwa, watafiti hao walisema uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI Scanners.

Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.

Mnamo mwaka wa 2010 mwanafizikia mshindi wa tuzo ya Nobel, Robert Richardson, alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.

Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na gesi ya Helium kuwa nyepesi kuliko ile ya Oxygen.

“Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI,”  alisema Chris Ballentine kutoka Chuo Kikuu cha Oxford.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles